Kamati ya Lishe ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imefanya kikao cha tathimini ya afua za lishe ya robo ya pili kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.
Akifungua kikao hicho Mkuu wa Idara ya Utawala na rasiliamali watu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Omary Mkangama amesema kuwa Halmashauri ya Handeni inatekeleza maagizo ya upatikanaji wa lishe kwa vitendo kwani lishe ni jambo muhimu kwa kila mtu na lishe bora inaaza tangu mtoto akiwa tumboni hivyo mama mjamzito anapaswa apate lishe bora kwa ukuaji wa afya ya akili ya mtoto.
Ili mwanafunzi ajifunze vizuri na watumishi wafanyekazi kwa weledi lazima wapate lishe bora. Alisema.
Kuhakikisha wanafunzi wanapata hasa chakula cha mchana wawapo shuleni kamati imeshauri kila shule kulima angalau heka tatu za mazao ya chakula na kutoa maelekezo kwa kamati za shule kuhakikisha zinasimamia kwa kila shule wanafunzi wanapata chakula cha mchana.
Pia kwenye kikao hicho zoezi la upimaji wa afya na uzito pamoja na ushauri wa kula lishe bora kwa jamii ilitolewa.
Bw. Omary Mkangama, Mkuu wa Idara ya Utawala na rasilimali watu wa Halmashauri ya Handeni.
Afisa Lishe wa Halmashauri ya Handeni Bi. Julia Chalo akiwasilisha taarifa ya lishe mele ya kamati ya lishe ya Halmashauri.
Afisa Mifugo Dkt. Key Amiri, (aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya idara ya mifuko kwenye kamati ya lishe.
Afisa Kilimo Bw. Athuman Malipula (aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya Idara ya kilimo mbele ya kamati ya Lishe.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa