Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Handeni yafanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kuangalia utekelezaji wa ilani ya Chama tawala.
Kamati hiyo iliyoongozwa na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Handeni Mh. Athumani Malunda ilifanya ukaguzi wa jengo la makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni linaloendelea kujengwa. Pia kamati hiyo ilikagua kiwanda cha kuchakata mihogo cha kina mama Jipemoyo klilichopo kata ya kitumbi.
Mwenyekiti aliwashukuru wajumbe wa kamati ya siasa kwa kufanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Halmashauri ya Handeni.
Pia aliwapongeza Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni pamoja na wafanyakazi wa Halmashauri kwa kuitekeleza vizuri ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa vitendo. Mwenyekiti huyo aliwakumbusha wajumbe Kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa hatari wa Korona (COVID 19).
Mh. Athumani Malunda katika kiwanda cha kuchakata mihogo cha kina mama jipemoyo kilichopo kata ya kitumbi alisema kuwa kumwezesha mwanamke sio kumpa pesa bali kumwanzishia mradi ndiyo utakaomwezesha kupata pesa ambazo ni endelevu.
Kwaupande wa Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe alimshukuru Mkurugenzi na wafanayakazi kwa ushirikiano wao katika utekelezaji wa miradi mbalimbali na kuweza kuifanya Handeni iwe na ongezeko la kimaendeleo.
Mkuu wa Wilaya alimuagiza Meneja wa wakala wa barabara mjini na vijijini (TARURA) Wilaya ya Handeni kurekebisha barabara inayoanzia kwenye barabara kuu (Chalinze-Segera) inayoelekea kwenye jengo la makao makuu ya ya Halamshauri. Mh Godwin Gondwe amemuagiza meneja wa TANESCO Wilaya ya Handeni kuhakikisha anaweka nyaya za umeme kwenye nguzo zilizisimikwa kuelekea kwenye eneo la ujenzi wa jengo la makao makuu ya Halamshauri ya Handeni.
Katibu tawala wa Wilaya ya Handeni Mh. Mwl Boniphace Maiga amewaelekeza Maafisa elimu wa Halmashauri kuandaa vitini vya maswali hasa kwa madarasa ya mitihani na kufanya mawasiliano na wazazi wa wanafunzi hao kuja kuchukua na kuwapelekea watoto wao wakayafanye maswali hayo na kuyarudisha kwa walimu kwaajili ya tathimini ya upimaji wa maendeleo yao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw.William Makufwe aliishukuru kamati hiyo kwa kufanya ziara ili kupima utekelezaji wa miradi katika Halmashauri yake. Pia Bw. Makufwe alisema mradi wa ujenzi wa jengo la makao makuu ya Halmashauri linaendelea vizuri mpaka sasa limefikia 20% na kueleza changamoto zinazozikabili ujenzi wa jengo hilo kuwa ni mvua na ubovu wa barabara inayopelekea vifaa vya ujenzi kushushwa eneo lingine na kuchukua usafiri mwingine na kuongezeka kwa gharama za ziada. Mkurugenzi Mtendaji amesema kuwa pesa za kuwawezesha kiwanda cha kuchakata mihogo cha kina mama Jipemoyo kilichopo kata ya Kitumbi zimetokana na mapanto ya ndani ya Halmashauri. Aidha Mkurugenzi amesema tayari kunamazungumzo yanaendelea kuhusu makubaliano na kampuni kutoka Dar es salaa itaingia mkataba na kiwanda hiko na kununua unga wa muhogo tani mia moja (100).
Kwapamoja wajumbe wa kamati ya siasa ya Wilaya ya Handeni wamemuelekeza Meneja wa TANESCO kupeleka umeme kwenye kiwanda cha kuchakata mihogo cha kina mama jipe moyo kilichopo kata ya kitumbi kwaajili ya kuongeza uzalishaji kiwandani hapo.
Mwenyekiti wa kamati ya siasa ya Wilaya ya Handeni Mh. Athumani Malunda aliyeshika karatasi akitoa ufafanuzi kwenye ujenzi wa jengo la makao makuu ya Halmashauri ya Handeni.
Mh. Athumani Malunda wa kwanza aliyetangulia akiwa na wajumbe wa kamari ya siasa ya Wilaya wakikagua barabara inayoelekea kwenye jengo la makao makuu ya Halmashauri ya Handeni.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni aliyetangulia mbele akitoa maelekezo ya ujenzi wa barabara inayoelekea kwenye jengo la makoa makuu ya Halmashauri ya Handeni.
Katibu tawala wa Wilaya ya Handeni Mh. Mwl Boniphace Maiga akifafanua jambo kwenye ujenzi wa jengo la makao makuu ya Halmashauri ya Handeni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe akitoa ufafanuzi wa ujenzi wa jengo la makao makuu ya Halmashauri ya Handeni.
Kamati ya siasa ya ya Chama cha Mapinduzi ya Wilaya ya Handeni ikiwa kwenye kiwanda cha kuchakata mihogo cha kina mama jipemoyo kilichopo kata ya kitumbi.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa