Mkuu wa Wilaya ya Handeni pia ni mwenyekiti wa kamati ya Ushauri ya Wilaya Mhe. Siriel Mchembe aongoza kamahi hiyo kufanya kikao maalum cha ushahuri Wilaya ya Handeni.
Mhe. Mchembe amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa namna anavyoipatia Wilaya ya Handeni fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali kwenye Wilaya ya Handeni akitolea mfano wa ujenzi wa madarasa Mkuu wa Wilaya amesema kuwa wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2022 wameingia darasani na hakuna mwananfunzi anayekaa chini kwa kukosa dawati hii kutokana na juhudi zake za kutoa fedha za UVIKO-19 ili zijenge madarasa amabayo yametatua changamoto za uhaba wa madarasa kwa Wilaya ya Handeni.
Kwa kupitia kikoa hiko Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Siriel Mchembe amewapongeza wadau wa maendeleo kwa michango yao mbalimabali kwa ajili ya maendeleo ya Halamashauri ya Wilaya ya Handeni.
Kwa kutambua michango ya wadau wa maendeleo kwenye Halmashauri kupitia kikao hiko cha ushauri Wilaya Mkuu wa Wilaya Mhe. Siriel Mchembe alitoa tuzo kwa wadau hao ambao ni pamoja na Shirika la maendeleo la World Vision Tanzania, Shirika la DORCAS, Shilika la AMREF, Shirika la CAMFED, Godmwanga Gems Ltd, Islamic Help na Tanzania Muslim Shia.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Siriel Mchembe amabaye ni mwenyekiti wa kamati ya ushauri Handeni akiongea kwenye kikao cha Ushauri maalum.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Handeni Mhe. Athumani Malunda akitoa neno kwenye kamati maalum ya Ushauri Wilaya ya Handeni.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mhe. Mussa Mwanyumbu (aliyesimama) akiongea kwenye kikao huko.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Saitoti Zelothe Stephen, akiongea kwenye kikao hiko.
Afisa Tarafa ya Mazingara Ngudu Amin Yassini wa kwanza kushoto akimsikiliza Mkuu wa wilaya kwenye kikao hiko.
Wajumbe wa Kikao cha ushauri wa Wilaya ya Handeni wakimsikiliza mkuu wa Wilaya ya Handeni.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa