Katibu tawala wilaya ya Handeni Mhe. Mashaka Boniphace Mgeta amefungua maadhimisho ya siku ya mkulima Handeni yaliyofanyika kwenye kijji cha Suwa kata ya Mazingara.
Mhe. Mgeta amemshukuru mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri na wafanyakazi wote wa Handeni kwa ushirikiano na kufanikisha siku ya mkulima pia amewapongeza wadau wa kilimo cha muhogo na taasisi zote za utafiti kwa juhudi kubwa za kuhakikisha wakulima wa muhogo wanalima kwa kutumia mbegu bora ili kupata mazao yenye tija kwaajili ya chakula na kujiongezea kipato na amewaagiza maafisa ugani wote kuwatembelea wakulima shambani ili kutoa ushauri wa kitaalam kwa wakulima.
Kwakuhitimisha Mhe. Mashaka Mgeta amewahasa wazazi kutumia kilimo chenye manufaa ili kuwasomesha watoto wao hususani wa kike na mzazi ambaye mtoto wake hajampeleka shule sheria za mtoto zipo na zitachukuwa mkondo wake na mapango wa elimu Handeni kila Tarafa kuwe na kidato cha tano na sita hivyo wazazi wapeleke watoto wao shule.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni Bw. William Makufwe amemshukuru Katibu tawala wa wilaya ya Handeni pamoja na wanachi waliojitokeza kushiriki kilele cha siku ya Mkulima Handeni.
Bw. Makufwe amesema kuwa ameanza kuhamasisha zao la muhogo wilaya ya Handeni tangu mwaka 2016 kutokana na njaa kwenye wilaya ya Handeni hivyo kwa kushirikiana na wataam wa Halmashauri wameondoa janga la njaa kwa kuhimiza kila familiya kulima heka tatu za muhogo kwa kufuata mashariti ya kilimo cha muhogo kuzingatia ushauri wa wataalam waliopo kwenye kila kata.
Kwakumalizia Bw. Makufwe amesema kuwa wawekezaji kutoka Dubai wanajenga kiwanda cha kuchakata muhogo kwenye Halmashauri ya Handeni na watahitaji tani 300 za muhogo kila siku kwaajili ya kiwanda hicho hivyo mahitaji ya muhogo ni makubwa ndani ya Handeni na nje kwani kila siku magari yanapekeka kuuza muhogo kwenye masoko ya Dar es Salaam.
Katibu tawala wilaya ya Handeni Mhe. Mashaka Mgeta, kulia aliyevaa koti akimsikiliza afisa kilimo wa Halmashauri ya Handeni aliyeshika karatasi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe wapili kushoto akisikiliza maelezo kuhusu ubora wa mbegu ya muhogo aina ya Pwani kutoka kwa mtafiti wa mazoa ya mizizi Dkt. Esther Masumba.
Afisa kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bw. Yibarila K. Chiza aliyesimama akiongea jambo kwenye maadhimisho hayo.
Dkt. Esther Masumba mtafiti wa mazao ya mzizi akielezea aina ya magonjwa yanayoshambulia zao la muhogo.
Mbegu ya Muhogo aina ya Pwani hutoa mazao zaidi ya tani hamsini (tani 50) kwa hekari moja.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa