Katibu tawala wa Mkoa wa Tanga Bi. Junica Omari amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ya sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na madarasa yaliyojengwa kwa fedha za Lipa kulingana na matokeo (EP4R) katika Halmashauri ya Handeni.
Bi. Junica Omari amekagua majengo ya madarasa katika shule za Kabuku sekondari, Shule ya msingi Kabuku nje, Shule ya msingi Kwedikwazu Mashariki, Shule ya sekondari Kisaza,Shule ya sekondari Kitumbi na Shule ya msingi Mhalango. Katibu tawala Mkoa wa Tanga Bi.Junica Omari amewapongeza walimu, watumishi wa Halmashauri, wazazi, wanafunzi na wadau wa elimu kwa jitihada za kuingeza ufaulu wa darasa la saba na kidato cha nne mwaka 2019.
Amesema matokeo mazuri yanaonesha kuwa Handeni wamejipanga kwa kufanya vizuri kwenye sekta ya elimu na amewakumbusha watumishi kuwa na mahusiano mazuri wawapo kazini kwakuwa maendeleo yanapatikana kwa ushirikaiano wa wafanyakazi wote
Bi. Junica Omari amewaasa watumishi kufanya kazi na kuacha kutafuta visingizio vya kuhama pale walipo sasa na ameongeza kuwa watumishi lazima wawe wabunifu wawpo kazini ili kutoa ufanisi mzuri na matokeo makubwa.
Afisa elimu mkoa wa Tanga Bi. Mayasa Hashim amemuambia katibu tawala mkoa wa Tanga kuwa uongozi wa Halamshauri ya Handeni pamoja na wafanayakazi wanafanya kazi kwa ushirikiano na wanatekeleza kwa wakati kila jukumu wanalopewa.
Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe amemueleza katibu tawala wa mkoa wa Tanga kuwa kwa sasa shule zote za Halmashauri ya Handeni zinapata chakula cha mchana kwakuwa kila shule inalima mihogo hekari tatu, mahindi hekari tatu kwaajili ya chakula na korosho hekari tatu kwaajili ya biashara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe amemshukuru Katibu tawala wa mkoa kwa kufanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo kwenye Halmashauri yake na kumuahidi kuwa yeye pamoja na wafanyakazi wote wa Halmashauri watasimamia kikamilifu miradi yote iliyopo kwenye Halmashauri hiyo.
MWISHO.
Katibu tawala mkoa wa Tanga Bi. Judica Omari kushoto akisalimiana na watumishi wa Halmashauri ya Handeni.
Bi. Judica Omari akinawa mikono kujikinga na korona alipowasili ofisi za Halmashauri ya Handeni.
Katibu tawala mkoa wa Tanga Bi.Judica Omari akikagua ofisi za muda za halamsahauri ya Wilaya ya Handeni.
Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh. Gondwin Gondwe mbele akimuongoza katibu tawala mkoa wa Tanga kukagua ofisi za muda za Halmashauri ya Handeni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe mwenye koti jeusi akitoa ufafanuzi mbele ya katibu tawala mkoa wa Tanga Bi.Judica Omari alipotembelea ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Handeni.
Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni wakimsikiliza Katibu tawala mkoa wa Tanga.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa