Katibu tawala wilaya ya Handeni Mhe. Mashaka Boniphace Mgeta akimwakilisha mkuu wa Wilaya ya Handeni amezindua baraza la wazee wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni na kuwashukuru wazee kwa ushirikino na umoja wao kwa maendeleo ya Handeni na Taifa kwa ujumla.
Akisoma maneno ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe.Toba Nguvila kwa wazee hao amesema kuwa anashukuru kuteuliwa kuwa mgeni rasmi na kuwapongeza Halmashauri ya Handeni kwa kuandaa na kukamilisha uundaji wa baraza la wazee na kusema kuwa jukumu la kuwatunza wazee ni la kwetu sote na wazee wapate huduma sawa na watu wote
Kwakumalizia Mkuu wa Wilaya ya Handeni amesema kuwa wazee ndiyo chachu ya maendeleo ya leo na mahitaji ya wazee yawe ni ya haki sio msamaha.
Kwa upande wa Katibu tawala wa Handeni Mhe. Mashaka Mgeta amempongeza Mkurugenzi Mtendaji pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Handeni kwa kugawa rasilimali fedha kwa wazee na kuandaa mazingira mazuri ya wazee kupata huduma ili nao waweze kunufaika na matunda ya nchi.
Pia Mh. Mgeta amesema kuwa miradi yote ya maendeleo kiwekwe kipengele cha kuwatunza wazee na amewakumbusha watumishi kuwapa kipaumbele wazee kwenye semina zinazowahusu na tuwaunganishe wazee wa Handeni na wazee wa nje ya Handeni.
Kabla ya kufungua baraza hilo katibu tawala Wilaya ya Handeni Mhe. Mgeta alisimamia uchaguzi wa viongozi wa baraza la wazee ambapo Mzee Ismail Mrope amechaguliwa kuwa mwenyekiti, Mzee Sufiani Mhando amechaguliwa kuwa katibu na Mzee Ally Kadege kuwa mweka hazina na kuwaapisha viongozi hao pamoja na kuwapa majukumu ya baraza hilo kwa wazee wa Handeni.
Afisa utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Charles Mwaitege amesema kuwa utambuzi wa wazee uwe endelevu kwani kila mara wazee wanaongezeka na watambulike kisheria na ameshauri kuwa kwenye hospitali, vituo vya afya na zahanati kuwepo na daktari maalum atakaye hudumia wazee ili wapate huduma nzuri.
Kwakumalizia Bw. Mwaitege ameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuwajali wazee na kuwaandalia mazingira mazuri ya kupata huduma za afya na kuwapunguzia ukali wa maisha kupitia mfuko wa TASAF.
Katibu tawala wa wilaya ya Handeni Mhe. Mashaka Mgeta aliyesimama akitoa maelekezo kwenye uzinduzi wa baraza la wazee.
Katibu tawala wa wilaya ya Handeni Mhe. Mashaka Mgeta kulia akimkabidhi nyaraka za ofisi mwenyekiti wa baraza la wazee wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Mzee Ismail Mrope.
Afisa utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Charles Mwaitege aliyesimama akifafanua jambo kwenye uzinduzi huo.
Afisa ustawi wa Jamii Bw. Jovin Gosbert kulia akimkabidhi katibu tawala wilaya ya Handeni taarifa ya ustwawi wa Jamii.
Baadhi ya wazee wa baraza la wazee wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni wakipokea malekezo kutoka kwa Katibu tawala wa wilaya ya Handeni.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa