Kikao cha Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) yafanyika Handeni DC
Kikao cha Jumuiya Tawala za mitaa (ALAT) ya kufunga mwaka wa fedha 2017/2018 ilifanyika jana tarehe 17/09/2018 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe
Kikao hicho cha jumuiya ya Tawala za Mitaa hufanyika kila robo ya mwaka kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya Halmashauri ambapo wajumbe wake ni wenyeviti wa Halmashauri zote za Mkoa, Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri zote za Mkoa na wawakilishi wawili wa Waheshimiwa madiwani kutoka Halmashauri zote za Mkoa.
Akifungua kikao hicho Mh. Godwin Gondwe alisema kuwa watendaji wakuu wa serikali wametoka kwenye serikali za mitaa hivyo amewaasa kusimamia shughuli za maendeleo mkakati katika Mkoa wetu wa Tanga ikiwepo ukusanyaji wa mapato pamoja na kero za wananchi na kwamba elimu ya suala la mapato liangaliwe kwa undani kuwe na mikakati mizuri ya ukusanyaji mapato na amesema sisi kama viongozi tutashirikiana kwa pamoja kuhakikisha kwamba mapato katika Mkoa wetu wa Tanga yanaongezeka kwani Tanga sasa hivi imekaa kimkakati kwa kuwa miradi yote ya kimkakati ya Taifa ipo Mkoa wa Tanga ikiwepo bomba la mafuta hivyo amewaasa wajumbe kuangalia fursa hizo na kutoa elimu kwa wananchi kwa pamoja ili waweze kukamata fursa zitakazotokana na bomba hilo la mafuta kama makampuni yaliyosajiliwa ya ulinzi katika maeneo yote ambayo bomba linapita, makampuni ya huduma ya chakula na sheria ndogo ya ulipaji wa kodi katika Halmashauri ambazo bomba hilo linapita pia.
Ameongeza kuwa sekta ya elimu pia tumejiwekea mikakati mbalimbali kama bank ya matofali ili kuhakikisha kutokuwa na uhaba wa madarasa na je hizo bank zimeanza kufanya kazi, na kama matofali yapo yanatumika, na lini itakuwa mwisho wa kutumia wa matumizi wa matofali hayo, hivyo basi tuone mpango mkakati tunatekeleza vipi kuhakikisha hatuna upungufu wa madarasa.
Katika suala la ufaulu Mh.Godwin Gondwe amesema kuwa Mkoa wetu wa Tanga bado ufaulu hauridhishi kabisa tunamkakati gani kwa wale watendaji walioko chini yetu kuhakikisha tunaondoka katika nafasi hiyo ya chini sana tuliyonayo tuwaze kwenda mbele katika sekta yetu ya elimu ili tupate ufaulu ulioenda juu zaidi.
Pia amesema mazao ya kimkakati kwa Mkoa wetu wa Tanga ikiwepo zao la mkonge na amesema kwamba mkonge bora zaidi umetoka mkoa wa Tanga na pia unahitajika kwa wingi Duniani kutokana na kuwa mbadala wa plastiki kwani plastiki itaondolewa kabisa na amesema pia mkonge ni zao bora kwani inavunwa mara mbili kwa mwaka baada ya kustawi kwa muda wa miaka mitatu “tumetumia asilia mbili ya mkonge wa Tanga bado tuna asilimia tisini na nane”alisema. Korosho, matunda pamoja na mihogo pia ni mazao yetu ya kimkakati na hivi vyote ni malighafi ya viwanda kama nchi yetu ilivyo ya viwanda kwa hiyo tujiwekee mpango mkakati mzuri ili Tanga tuweze kwenda juu zaidi.
Alitimisha kwa kuhimiza Halmasauri kutoa michango ya vikao vya jumuiya ya tawala za mitaa(ALAT) kwa muda ili vikao viweze kufanyika kwa wakati, Pia aliwapongeza Wakurugenzi wapya walioteuliwa ili kusukuma gurudumu la maendeleo ya Taifa.
Mwenyekiti wa jumuiya ya Tawala za mitaa(ALAT) Mkoa wa Tanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mh.Ramadhani Diliwa amesema kuwa lengo kubwa la vikao vya ALAT ni uboreshaji wa ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri zetu kulingana na malengo waliyojiwekea ambapo baadhi ya Halmashauri kama Kilindi na Lushoto zimevuka lengo lakini baadhi zina asilimia sabini hadi themanini.
Mh.Diliwa amesema lengo lingine ni kuwainua wakulima wa chini ili kulima mazao ya kimkakati ya biashara kama mihogo na Korosho kwani imeonenekana inafanya vizuri katika Halmashauri zetu na kwamba Handeni sasa imeingia kwenye mchakato wa kujenga kiwanda cha kuchakata mihogo katika Kata ya Kwedizinga kwa hiyo tuone namna gani ambavyo wakulima wa Halmashauri zingine za Mkoa wa Tanga watanufaika pia na kiwanda hicho.
Makamu mwenyekiti wa jumuiya ya tawala za mitaa (ALAT) Mkoa Mh. Mustafa Mhina alimshukuru mgeni rasmi kwa kuja kufungua kikao hicho na pia kuwakumbusha wajibu wao kama viongozi wa Halmashauri na pia kuwakumbusha Wakurugenzi nafasi zao ili kumsaidia Mh.Raisi katika suala zima la kuisukuma nchi hii katika uchumi wa Viwanda.
Pia alitoa rai yake kwa mgeni rasmi ya kuwa na bodi machungwa kama ambavyo kuna bodi ya mazao mengine ikiwepo bodi ya Korosho, bodi ya Mkonge na bodi ya tumbaku ili tuweze kuimarisha soko kwani machungwa yamekuwa yakiharibika na wakulima wanapata hasara sana na kukata tamaa.
Katibu wa kikao cha jumuiya ya tawala za mitaa (ALAT) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw.William Makufwe aliwaeleza wajumbe miradi ya Handeni ambayo wangetembelea lakini kutokana na ufinyu wa muda walishindwa ni pamoja na kiwanda cha kuchakata mahindi,matunda,kutengeneza unga wa lishe na chakula cha mifugo kilichopo kata Segera, upanuzi wa miundo mbinu ya majengo ya kituo cha afya Kabuku ikwepo jengo la wamama,chumba cha upasuaji, maabara,chumba cha kufulia nguo, chumba cha maiti, na nyumba ya mganga, mradi wa upimaji ardhi na urasimishaji makazi katika kata za Kabuku,Segera na Mkata, kutembelea shamba la kulima bora wa mihogo aliyeko Kata ya Kitumbi pamoja na kutembelea shamba la korosho.
Aidha wajumbe wa kikao hicho walipokea na kupitisha mapendekezo ya sekretariati ya ALAT Mkoa ambayo yatapelelekwa kwenye mkutano wa ALAT ngazi ya Taifa yaliyowasilishwa na katibu wa ALAT Mkoa wa Tanga Bw.William Makufwe. mapendekezo hayo ni:
Serikali kuu iridhie kuongezwa kwa posho za waheshimiwa madiwani kutokana na shughuli kubwa wanayofanya.
ALAT Mkoa inaiomba serikali kuu kuleta Ruzuku ya Mapato Mengineyo (OC) zikiwa timilifu na kwa wakati ili zisaidie katika uendeshaji wa Halmashauri husika.
Kutokana na ufinyu wa bajeti za Halmashauri ALAT Mkoa inaiomba Serikali kuu kuleta fedha kwaajili ya uchaguzi kulingana na mahitaji ya kila Halmashauri husika.
Kwa kuwa Ruzuku ya Miradi ya maendeleo (LGDG) imekuwa ikiunga mkono nguvu za wananchi ALAT Mkoa inaiomba Serikali kuu kuendelea kutoa ruzuku hiyo mpaka miradi ya kimkakati itakapoimarika kwa Halmashauri zote.
MWISHO
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa