Kuelekea maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imepanda miti ya Matunda na aina nyingine mbalimbali kwenye eneo la shule ya Msingi Kwedigunda.
Zoezi hilo la upandaji miti limeongozwa na Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu wa Halmashauri ya Handeni Bw. Omary Mkangama.
''MITI YANGU, MAZINGIRA YANGU''
Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru ni '' Amani na Upendo ni Nguzo ya Maendeleo Yetu''
Mkuu wa Idara ya Utawala na rasilimali watu wa Halamshauri ya Handeni Bw. Omary Mkangama, akirudishia Udongo mara baada ya kupanda Mti wa Muembe.
Mkuu wa Idara ya Misiti na Maliasili Bw. Nepoleani Mlowe ( aliyevaa T-shirt ya Njano) akiweka mbolea kwenye shimo ili kupanda mti
Wakuu wa Idara na Vitengo walijitokeza kwa ajili ya kupanda miti hii leo.
Kaimu Afisa wa Maeneleo ya Jamii, Bi. Amina Waziri akihamasisha wanafunzi watunze miti hiyo na kuyapenda mazingira yao.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa