Maadhimisho ya juma la elimu kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Chanika Wilayani Handeni, Mkoa wa Tanga kwa siku tano kuanzi tarehe 27-31/05/2019 yenye kauli mbiu inayosema ELIMU BORA HAKI YANGU yamefungwa rasmi leo na Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI Bw. Tixon Nzunda.
Wakati akufunga maadhimisho hayo Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI Bw. Tixon Nzunda alisema maadhimisho haya yana lengo la kujitathmini na kupongezana kwa hatua nzuri tuliyopiga katika sekta ya elimu pamoja kujadili kwa uwazi changamoto zinazoikabili sekta ya elimu na kuona namna bora zaidi ya kwenda mbele.
Akibainisha shughuli zinazofanywa na serikali chini Mh. Raisi wa jamhuri wa muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ili kuhakikisha elimu bora inapatikana kwa wanafunzi amesema serikali imetoa elimu bila ada na kuondoa vikwazo vyote mtoto wa Tanzania anavyokutana navyo ili aweze kupata elimu bila kujali hali zao walizonazo na aliwataka viongozi wa Wilaya zote nchini kuhakikisha katika undikishaji wa wanafunzi wanazingatia watoto wenye mahitaji maalumu.
Ili kuendelea kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi kusoma Bw. Nzunda amesema serikali tayari imeshapeleka zaidi ya shilingi bilioni 2.2 katika shule mbalimbali kwa ajili ya ukamilishaji wa miundombinu ya maboma kwa shule za msingi ambapo fedha hizo zitakamilisha madarsa 177 na shilingi bilioni 29.9 kwa shule za Sekondari, Aliwaelekeza viongozi wa Mkoa na Wilaya kuhakikisha fedha zinakwenda kufanya kazi iliyopagwa kwa wakati ili kupunguza mrundikano wa wanafunzi.
Kufuatia changamoto ya upungufu wa walimu amesema serikali inalifanyia kazi suala hilo na imeanza kwa kuwaajiri walimu zaidi ya 4,749 kwa lengo la kupunguza upungufu wa walimu nchini na asema kwa upande wa Sekondari hatuna upungufu wa walimu wa sanaa ila wanaziada wa walimu zaidi ya 12000 na kutoa maelekezo ya kuwapeleka katika shule za msingi ili kuongeza ikama, amesema sehemu ya fedha ya tekeleza kulingana na matokeo zitumike kuwalipa walimu hao watakao hamishwa.
Aidha,Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI aliwataka Wakurugenzi wa Halmashauri wahakikishe fedha za tekeleza kulingana na matokeo zinakwenda kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa ikiwepo kujenga miundo mbinu, kuhuisha takwimu za elimu, uhamisho wa walimu ili kurekebisha ikama na kufuatilia miradi elimu msingi na pia amewataka Wakurugenzi hao kuhakikisha mishara ya walimu waliopandishwa daraja inabadilishwa kama ilivyoagizwa.
Alihitimisha kwa kuwashukuru wadau elimu na wadau wa maendeleo wakiwepo taasisi ya kiraia, World Bank, ubalozi wa Sweden, Marekani na Uingereza kwa kufadhili zaidi ya shilingi milioni 260 katika sekta ya elimu na kuwahakikishia fedha hizo kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa “kila shilingi mnayotupa inakwenda kufanya kazi iliyokusudiwa” alisema.
Mwenyekiti wa bodi ya Mtandao wa elimu Tanzania(Ten MeT) ambao pia ni wafadhili wa maadhimisho ya juma hilo la elimu Bw. John Kalage akisoma taarifa alisema wanatoa sehemu ya muda wao ili kuhamasisha jamii na hata kutoa mchango pale wanapoweza ili kuunga mkono jitihada za Mh. Raisi ya kutoa elimu bora bila malipo kwa wanafunzi wote wa Tanzania wakiwepo wenye mahitaji maalumu. Amesema tangu mtandao huo uanze kufanya kazi haya ni maadhimisho ya 16 na wameona matokeo chanya kwa kuwa kila sehemu walipoadhimisha uhamaishaji ulifanyika na ufaulu wa wanafunzi kuongezeka
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe alisema Handeni kitaaluma inaendelea kupanda kutokana kila mwaka wastani wa ufaulu kuongezeka kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2016 kwa kupata 65% , mwaka 2017 73% na 2018 81.6% na kuweka makubaliano yakifikia asilimia 100 kwa darasa nne na kidato cha pili na kufikia asilimia 95 kwa darasa la saba na kidato cha nne kwa kuwa shule kwa sasa zina chakula hivyo hakutakuwa na utoro wa rejareja kwa wanafunzi.
Gondwe amesema Wilaya ya Handeni imepokea milioni 300 kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma na kwamba katika ukamilishaji maboma hayo wameshafikia 95% na hizo asilimia zilizobaki watasimamia ili yaweze kukamilika kwasababu wao ni watekelezaji na amesema wabunge pia wamechangia katika miundo mbiu hiyo ambapo kila mbunge amechangia zaidi ya milioni 20 ili kuhakikisha elimu bila malipo inakaa sawasawa.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi TAMISEMI Bw. Tixon Nzunda akizungumza wakati wa kufunga maadhimisho ya juma la elimu
Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI kushoto Bw. Tixon Nzunda na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe wakiongoza maandamano
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Gondwe akizugumza
Baadhi ya mabango yaliyobebwa na wanafunzi yakiwa ujumbe mbalimbali
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa