Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imepongeza na kutoa zawadi kwa shule kumi za Msingi na moja Sekondari kwa kufanya vizuri kwenye mitihani ya darasa la saba na kidato cha nne mwaka 2016. Zawadi hizo zilitolewa kwenye kilele cha maadhimisho ya juma la elimu yaliyofanyika kiwilaya Wilayani Handeni kwenye shule ya Msingi Kabuku nje.
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Handeni ambaye pia alikuwa mgeni rasmi Mh. Godwin Gondwe aliwapongeza walimu na wadau wengine wa elimu kwa kazi nzuri wanazofanya na wanazoendelea kufanya katika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora.
“elimu ni ufunguo wa maisha na kwamba Handeni hakuna mtoto mjinga, wazazi na walezi himizeni watoto kutumia fursa ya Elimu bure inayotolewa na Raisi wa Tanzania” Alisema.
Aidha ameeleza kuwa atahakikisha fedha zinazohusu madai ya walimu zinapofika Halmashauri zinawafikia walengwa kwa wakati uliopangwa. Aliwataka wakuu wa shule na Maafisa elimu Kata kusimamia haki ya msingi ya wanafunzi kupata elimu wanayostahili.
kwa maelezo zaidi soma hapa.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa