Mradi wa Boost unatarajiwa kuboresha mazingira ya Ujifunzaji na Ufundishaji, ujuzi na ubora wa walimu katika ufundishaji pamoja na kuimarisha upatikanaji wa rasiliamali za utoaji wa huduma za elimu ngazi ya Halmashauri.
Akifungua mafunzo elekezi ya utekelezaji wa mradi wa boost kwa wajumbe wa timu za utekelezaji wa Mikoa na Halmashauri kutoka Tanga na Kilimanjaro, Afisa Elimu Mkoa wa Tanga Bi. Newaho Mkisi amesema thamani ya Mradi wa boost ni Triliani 1.15 kwa nchi nzima ambapo fedha hizo zitatolewa na Serikali kwa Kushirikaina na Bank ya Dunia kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 12,000 kwa shule za Awali na Msingi za Serikali hapa nchini kwa kipindi cha miaka mitano kwenye maeneo yenye upungufu na msongamono wa wanafunzi pamoja na kununua vifaa vya tehama na ujenzi wa vituo vya kutolea mafunzo kwa walimu.
Bi. Mkisi amewataka washiriki wa Mafunzo hayo kuzingatia weledi na ushirikiano kwenye Halmashauri zao katika utekelezaji wa maradi huo.
Akifunga mafunzo hayo ya siku mbili Mkurugenzi wa Elimu Maalum, Elimu nje ya mfumo rasmi na elimu ya Michezo kutoka TAMISEMI Bw. Julius Migea amemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Dkt. Smia Suluhu Hassan kwa kuijali kwa kipekee sekta ya elimu kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa na ujenzi wa mabweni kwa wananfunzi wenye mahitaji maalum.
Bw. Migea ameongeza kusema kuwa Halmahsuri zote zinawajibu wa kusimamia miradi yote ya miundombimu ya madarasa inayotekelezwa kwenye maeneo yao kwa weledi kulingaanoa na thamani ya fedha kulingana na ubora na kukamilisha kwa wakati.
Aidha kila mmoja kwa nafasi yake akawajibike kwa ajili ya kutekeza mradi huu wa boost kwenye maeneo yao kulingana na taaluma zao.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa matokea yaliyokubaliwa lazima yafikiwe kwa kuzingatia sheria kanuni na miongozo katika kutekeleza mradi huu wa BOOST.
Pia mradi huu sio wa mtu mmoja mmoja wataalam wote washirikiane kwa ajili ya kufikia malengo yaliyokusudiwa na kutobadilisha shule au miundombinu kwa shule zitakazobainishwa zenye matatizo ya miundombinu. Amesema Migea.
Mkurugenzi huyo ametoa rai kwa wataalam kushirikiana na wazazi kwenye zoezi zima la uandikishaji wa wanafunzi kuanza darasa la awali na darasa la kwanza ili miradi itakayojengwa iweze kutumika ipasavyo. Tamisemi itafuatailia hatua zote za utekelezaji wa mradi huu na kuchukuwa hatua stahiki kwa wakati kwa miomgozo, sheria na makubaliono.
Mafunzo hayo ya siku Mbili yamefanyika katika shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe yakiwakutanisha wataalam 231 wa kada ya Elimu, Mipango, Uhasibu, Tume ya utumishi wa walimu wathibiti ubora wa elimu pamoja na maafisa habari kutoka Halmashuri 11 za Mkoa wa Tanga na Halmashauri 7 kutoka Mkoa wa Kilimajaro.
Mkurugenzi wa Elimu Maalum, Elimu nje ya mfumo rasmi na elimu ya Michezo kutoka TAMISEMI Bw. Julius Migea akiongea kwenye mafunzo hayo.
Wajumbe wa Mafunzo wakimsikiliza Bw. Migea
Washiriki wakiwa wanapata Mafunzo.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa