Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mpinduzi ya Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga amefanya ziara Mkoa wa Tanga na kutembelea Miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa Amewashukuru Wanahandeni kwa mapokezi makubwa hasa akinamama wamejitokeza kwa wingi sana.
Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha Milioni 250 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya Sindeni na amewahasa viongozi wa Handeni kuwa fedha hizo zitumike vizuri kwa mujibu wa matumizi yaliyokusudiwa kama ilivyoelekezwa bila mapungufu yoyote na Mkoa wa Tanga ni Mkoa unaotekeleza vizuri Ilani ya Chama Cha Mapinduzi hivyo kazi hii itasimamiwa vizuri na kukamilika kwa wakati ili wananchi wa Sindeni na Handeni kwaujumla wapate kituo cha afya na huduma pia.
Kwakumalizia Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka wananchi kujitokeza kwenye Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 ili wahesabiwe na Serikali iweze kupata idadi sahihi na kupanga mipango ya maendeleo pia amewakumbusha wananchi kujitokeza kwenda kupata chanjo ya ugonjwa wa uviko 19 kwani maradhi hayo bado yapo na selikali imeleta chanjo bila gharama yoyote.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mpinduzi ya Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akipanda mti kwenye eneo la ujenzi wa kituo cha Afya Sindeni.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Adam Kigoma Malima amemshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga kwa kufanya ziara kwenye eneo la ujenzi wa kituo cha Afya Sindeni na kushiriki ujenzi wa jengo hilo.
Mkuu wa Mkoa amesema watausimamia na kufuatilia ujenzi huo na kuhakikisha ndani ya miezi Mitatu jengo la wagonjwa wa nje, Maabara na kichomea taka vitakuwa vimekamilika.
Mhe. Malima amewaahidi wananchi wa Sindeni kuwa baada ya miezi mitatu maji na umeme vitakuwa vimefika kwenye kituo cha afya Sindeni na wananchi watapata huduma hizo kituoni hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Adam Kigoma Malima.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Handeni Dkt. Kanansia Michael Shoo akisoma taarifa ya upatikanaji wa huduma ya afya Handeni mbele ya Makamu Wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mpinduzi ya Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga amesema tunatoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha kiasi cha Shilingi Milioni mia mbili na hamsini kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya Sindeni. Tunatambua haya ni matokeo ya juhudi kubwa za Rais wetu kupitia makusanyo ya Tozo za miamala ya simu na sisi Handeni ni wanufaika wa tozo hizo.
Dkt. Kanansia ameongeza kusema kuwa kituo cha afya Sindeni kinatarajia kuhudumia wakazi wapatao 68,754 na ujenzi wa kituo hiki kitasogeza huduma karibu na wananchi sawasawa na matakwa ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2020-2025 yenye lengo la kuimarisha na kuongeza vituo vya kutolea huduma za Afya nchi nzima.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Handeni Dkt. Kanansia Michael Shoo akisoma taarifa.
Baadhi ya Madiwani pamoja na wananchi wa Sindeni waliojitokeza kwenye ziara hiyo.
Wananchi waliojitokeza kwenye Ziara ya Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa