Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Handeni,.
Mama Samia Suluhu ameweka jiwe la msingi kwenye jengo la makao makuu ya Halamashauri ya Handeni linaloendelea kujengwa eneo la Mkata pia amefungua kiwanda cha kusaga mahindi na cha kutengeneza juisi kilichopo Segera.
Akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa jengo la makao Makuu ya Halmashauri, Mama Samia Suluhu amewashukuru wanahandeni kwa kukirudisha madarakani Chama Cha Mapinduzi hivyo watakamilisha ahadi zote zilizopo kwenye ilani ya chama na kukamilisha miundombinu yote pamoja na jengo hilo na amewapongeza Halmashauri kwa usimamizi wa fedha zinoletwa kwaajili ya maendeleo ya Handeni.
Aidha Makamu wa Rais Mhe. Samia amewaasa Watanzania kushikamana na kufanaya kazi ili kujenga uchumi kuhakikisha Tanzania inasonga mbele.
Uanzishwaji wa mji mdogo Kabuku Mama Samia amesema Serikali ya mkoa na Wilaya ianze mchakato kisha wapeleke taarifa kama imekidhi vigezo Kabuku utakuwa mji mdogo.
Kwakuhitimisha Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu amesema changamoto zote zilizopo kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi na ahadi ambazo Rais ameahidi zitatekelezwa zote na kuwahakikishia wananchi wote wanapata maji safi na salama, huduma za afya bora na fursa ya kupata elimu bure.
Kwaupande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe akitoa taarifa ya ujenzi huo mbele ya Makamu wa Rais, ameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri ya Handeni na mpaka sasa ujenzi umefikia 40%.
Bwana Makufwe amesema walipofanya mapitio ya gharama za ujenzi ili kumpa mkandarasi kujenga jengo gharama za ujenzi ilikuwa billion 7.8 baada ya kuamua kutumia “force account” ujenzi utakamilika kwa bilioni 5.3 na kuokoa kiasi cha biliaoni 2.5 ambazo zitatumika kwenye maeneo mengine.
Aidha Mkurugenzi Makufwe amesema kuwa Halmashauri inapokea fedha za ujenzi kwa awamu na mpaka sasa imepokea kiasi cha Bilioni 2 kwakutumia “force account” Halmashauri imeokoa kiasi cha Millioni 500. Ameongeza kusema kuwa jengo hilo la makao makuu ya Halmashauri litakapokamilika litakuwa na ofisi 209, kumbi mbili za mikutano zitakazochukuwa watu 200 kila ukumbi na idara zote zitakuwa pamoja ili kurahisiha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Kwa kumalizia Bw. Makufwe amezitaja changamoto kwenye ujenzi wa jengo hilo amesema kuwa ubovu wa barabara kutoka barabara kuu kwenda eneo la ujenzi ilisababisha gari zilizokuwa zinapeleka vifaa kushindwa kufika eneo la ujenzi na kushusha vifaa hivyo eneo lingine na kusababisha gharama za zaidi na mvua kubwa zilizonyesha mwanzoni mwa mwaka 2020 ilisababisha kazi ya ujenzi kuchelewa.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu akipanda mti kwenye kiwanda cha kusaga mahidi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni wapili kulia aliyeshika kitabu Bw. William Makufwe akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo la makao makuu ya Halmashauri mbele ya Makamu wa Rais.
Mhandisi John Mshahara, aliyevaa kofia ngumu akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo la makao makuu ya Halmashauri mbele ya makamu wa Rais.
Wakuu wa Idara pamoja na wananchi waliojitokeza wakimsikiliza Makamu wa Rais.
Jengo la makao makuu ya Halmashauri linaloendelea kujengwa.
Muonekano wa barabara inayoelekea kwenye ujenzi wa jengo la makao makuu ya Halmashauri kabla ya kufanyiwa matengenezo.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa