Tunamshuku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani ametupa hali ya upendeleo kwenye sekta ya elimu, wanafunzi wote kuanzia darasa la awali mpaka kidato cha sita wanasoma bure bila kulipa ada.
“Wanamafunzo ninyi ndiyo viongozi ambao mmekabidhiwa dhamana kubwa katika sekta ya elimu na utoaji wa Elimu bora,pia ninyi ndiyo nguzo muhimu ya maendeleo katika nchi yetu na kwakuwa elimu bora husaidia upatikanaji wa rasilimali watu wenye maarifa na ustadi katika nyanja mbalimbali hivyo husaidia kuleta maendeleo katika nchi yetu."
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Elimu ya Awali na Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bi. Rehema Nyoka wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya Uundaji wa Jumuiya za Umoja wa Wazazi na Walimu (UWAWA) yanayofayika kwa siku tatu kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Kuanzishwa na kutekelezwa kwa UWAWA kutaleta matokeo chanya ya Elimu kwa kuwa walimu na wazazi watajenga hisia za umiliki wa shule, kusaidia,kuimarisha miundombinu jumuishi, kuchangia katika mipango ya shule na kuongeza ushirikiano wa kamati za na shule.
Aidha Bi. Rehema Nyoka amesema kuwa kamati hizo zinapaswa kusimamia nidhamu za watoto wetu na changamoto zote kuanzia darasa la awali zikatatuliwe,kupitia mafunzo haya tukasimamie na kudhibiti swala la utoro na kupandisha mahudhurio ya wanafunzi shuleni pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya shule na kutekeleza zoezi zima la upatikanaji wa chakula shuleni. Bi Rehema Amesema.
Mafunzo hayo yanawezeshwa na Mradi wa Shule bora unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Uingereza (UK AID) na kutekelezwa kwa pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Elimu na Ofisi ya Raisi TAMISEMI kwa lengo la kutengeneza ushirikiano wa wazazi na walimu kwenye masuala ya ufundishaji na ujifunzaji katika elimu ya Awali na Msingi. Mafunzo hayo yanajumuisha Maafisa elimu wa Kata, wenyeviti wa Kamati za shule pamoja na walimu wakuu wa Shule za Msingi.
Sasa hivi kuna janga kubwa sana la watoto kulawitiwa,kupitia Mradi wa Shule Bora twende kama UWAWA tukasimamie na kukemea katika shule zetu jambo hilo tusimamie maendeleo ya taaluma na kupandisha ufaulu kwenye matokeo ya madarasa yote ya mitihani.
Bw. Shabani Kilamo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Kwamwanamangale iliyopo Kata ya Mazingara ameishukuru Serikali kwa kupitia Mradi wa shule Bora, amesema mafunzo hayo yamewaongezea ushirikiano kati ya walimu na wazazi ambao utasaidia kukomesha utoro na kuboresha mazingira ya wanafunzi kwenye suala la ujifunzaji hasa kuhakikisha chakula kinapatikana shuleni.
Bi. Rehema Nyoka, Mkuu wa Idara ya Elimu ya Awali na Msingi wa Halmashauri ya Handeni.
Bi. Rachel Mbelwa, aliyesimama mkuu wa idara ya Mendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Handeni.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa