Katika kuhamasisha vijana kujishughulisha na shughuli za maendeleo hususani kilimo mashindano ya mpira wa mguu na mpira wa pete UCHUMI CUP yamefunguliwa rasmi kwa ngazi ya robo fainali na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Handeni mapema mwishoni mwa wiki.
Akifungua mashindano hayo kwenye viwanja vya Kigoda Stadium Kaimu Katibu Tawala Wilaya Bi.Upendo Magashi alisema kuwa michezo ni furaha na amani hivyo fursa hiyo itumike kukuza vipaji lakini pia kujiunga katika vikundi vya uzalishaji hususani kilimo ukizingatia Handeni shughuli kuu ni kilimo.
Aliongeza kuwa lengo kuu la mashindano hayo ni kuhakikisha vijana wanatumia vipaji walivyonavyo katika kuhakikisha wanainua uchumi wao na kuendana na falsafa ya Mh. Rais ya HAPA KAZI TU!.
Kwa upande wake mratibu wa mashindano Bw. Baraka Nkatura alisema kuwa Mashindano yalianzishwa na Mkuu wa Wilaya Mh. Godwin Gondwe na kuamua kuyatumia kwenye msimu huu wa kilimo ili kuhamasisha vijana kutumia vipaji vyao kujiinua kiuchumi.
“Tunaamini mbali ya kukuza mahusiano baina yetu, tutaweza kubadilishana uzoefu utakaotusaidia kukuza vipaji vyetu na kujiinua kiuchumi” alisema Mratibu.
Upatikanaji wa timu zilizoshiriki Robo fainali ulianzia ngazi ya Tarafa tarehe 20/11/2017 ambapo, Tarafa 7 zilishiriki kutoa timu mbilimbili zilizoingia kwenye robo fainali na timu 2 alikwa moja kutoka jamii ya wamasai na ya pili kutoka Kabuku. Jumla ya timu 18 zimeingia ngazi ya mashindano ya robo fainali.
Aidha, baada ya kupatikana timu 18 kutoka kila Tarafa iliundwa mechi ya makundi kwa timu za ( Mjini Chanika kundi A, Misima B, Mkata C na Kabuku D). washindi wawili waliopatikana katika kila kundi waliingia robo fainali na kufanya timu shiriki 8.
Mpaka tarehe 4/2/2018 timu 4 zimecheza robo fainali , mchezo kati ya kurugenzi Fc na Nyikani walitoana 2-1, Ambapo Kurugenzi FC iliwafunga Nyikani FC bao 2 kwa mojo. Dakika ya 5 mchezaji John kutoka Nyikani FC alifunga goli la kuongoza na baadae mchezaji Nguruko kutoka Kurugenzi FC alisawazisha goli dakika ya 30 kabla ya mapumziko. Mchezaji Peter aliifungia Kurugenzi FC kwa shuti nje ya 18 Dakika ya 70 na kufanya bao la pili.
Mechi zinazocheza Robo fainali kwa lengo la kupata washiriki wa nusu fainali na fainali ni Kurugenzi FC vs Nyikani FC, Vibaoni United vs Kwamkono FC, Mtazamo United vs Ndolwa United na Umoja FC Vs Kwapara FC ambapo mwisho wa mashindano ya robo fainali ni 6/2/2018. Nusu fainali itachezwa tarehe 8-9/2/2018 na Finali itachezwa tarehe 11/2/2017.
Mashindano haya yamebeba kauli mbiu ya “Kipaji changu mtaji wangu” mbapo Mshindi wa kwanza atapa zawadi ya Kombe, pesa taslimu Tsh.500,000/=,medali za dhahabu, jezi seti moja na mipira mitatu. Mshindi wa pili atapata pesa taslimu Tsh.300,000/=, medali za fedha(Silva), jezi seti moja, mpira mmoja. Na mshindi wa tatu pesa taslimu Tsh.200,000/=,medali za shaba (Brons), jezi seti moja na mpira mmoja.
Washindi wa mpira wa Pete , mshindi wa kwanza atapata fedha taslimu Tsh.500,000/=, mshindi wa pili Tsh.300,000/= na mashindi wa tatu Tsh.200,000/=.
Kaimu Katibu Tawala Wilaya Bi. Upendo Magashi Akifungua mashindano ya robo fainali kwenye viwanja vya kigoda jumamosi tarehe 3/2/2018 kwa kuhamasisha vijan kujiunga kwenye vikundi vya uzalishaji hususani kilimo.
Mratibu wa mashindano akizungumza na wachezaji wakati wa ufunguzi wa mashindano ya robo fainali kwenye viwanja vya kigoda jumamosi
Timu ya Vibaoni United kabla ya kuanza mashindano dhidi ya Kwamkono united.
Timu ya Kwamkono United katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mchezo.
wachezeshaji wa mpira wakiwa katika picha ya pamoja na mratibu wa mashindano wa kwanza upande wa kulia Bw. Baraka Nkatula.
mapambano baina ya Vibaoni united na Kwamkono United yakiendelea viwanja vya Kigoda.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa