Mbunge wa jimbo la Handeni vijijini Mh. Mboni Mhita akabidhi gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) kituo cha afya Kabuku. Amesema lengo la kuomba gari hilo kutoa msaada kwa wananchi kupelekwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na kuitekeleza ahadi yake aliyoiahidi ya kuleta gari katika kituo cha afya Kabuku.
Akitoa shukrani zake kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mh. Mboni Mhita amempongeza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni kwa kazi nzuri anayoifanya Handeni na ushirikiano wake na ofisi ya mbunge kwa kutekeleza vizuri ilani ya Chama Cha Mapinduzi. Pia amempongeza kusimia suala la elimu Handeni kiwango cha elimu kimepanda mpaka kufikia 87% ya ufaulu kwa matokeo ya darasa la saba mwaka 2019.
Mh. Mboni Mhita amewashukuru wataalam wa Halmashauri ya Handeni kwa kusimamia fedha za maendeleo zinazoletwa kwenye Halmashauri na kuwapongeza wahudumu wa afya kwa kazi kubwa wanayoifanya. Amesema ameahidi kiasi cha milioni mia mbili (200M) kwaajili ya zahanati ya Segera na milioni mia nne (400M) kwaajili ya zahanati ya Kwamsisi.
Ameongeza kuwa ameshawapata wadau wa Afya kutoka Marekani ambao watampatia kontena mbili za vifaa tiba kwaajili ya kusaidia wagonjwa wa Handeni.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Handeni Bw. William Makufwe akimshukuru mbunge kwa kutekeleza majukumu yake kwa wananchi kwa kuleta gari la wagonjwa, amesema vituo vya afya nchi nzima ziko 352 na gari zilitolewa 50 hivyo ni juhudi kubwa iliyofanywa na mbunge mpaka kituo cha afya Kabuku kupata gari la wagonjwa.
Mh. Makufwe amesema kuwa walipata milioni mia nne (400M) kwaajili ya ujenzi wa majengo ya kituo cha afya Kabuku lakini wao kama Halmashauri wameongezea Milioni thelathini (30M) ili kuongezea umaliziaji wa majengo hayo. Pia Halmashauri wametoa kiasi cha Shilingi milioni hamsini na mbili (52M) kwaajili ya kujenga mifumo ya maji na kuweka umeme katika kituo cha afya Kabuku.
Alihitimisha kwa kusema kuwa Halmashauri imemepata milioni mia tano (500M) kwaajili ya umaliziaji wa jengo la hospitali ya Halmashauri inayojengwa Mkata na kwa bajeti ijayo tumetengewa kiasi cha bilioni 1.5 kwaajili ya hospitali ya Halmashauri na milioni mia tano hamsini (550M) kwaajili ya kujenga majengo katika kituo cha afya Kabuku.
Mganga mkuu wa kituo cha afya Kabuku Dr Lukas Masele amemshukuru mbunge kwa kuona umuhimu wa kuleta gari la kisasa la kubebea wagonjwa kituo cha afya Kabuku pia amempongeza mkurugenzi mtendaji kwa kuwa msikivu kwa kutoa ushirikano wakati wowote unapohitajika.
Mbunge wa Handeni vijijini Mh. Mboni Mhita aliyesimama akiongea kwenye zoezi la kukabidhi gari kituo cha afya Kabuku.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe kulia akiwa pamoja na viongozi wa kata ya kabuku wakiomba dua wakati wa zoezi la kukabidhi gari.
Afisa utumishi wa Halmashauri ya Handeni Bi. Fatuma Kalovya akisisitiza jambo kwenye zoezi la kukabidhi gari.
Mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Dr. Ipyana Mwandelile akitoa shukrani kwa mbunge kwa kupokea gari la kubebea wagonjwa Kituo cha afya Kabuku.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa