Rais wa Jamhuri ya muungano wa TannzaKia Dk. Joseph Pombe Magufuli ametoa siku 15 kufanyika uchunguzi wa fedha kiasi cha shilingi milioni 500 zilizotolewa kwaajili ya ujenzi wa Hospitali ya Mkata kufuatiwa kuwepo na taarifa za kufuja matumizi ya fedha hizo.
Rais ametoa rai hiyo leo alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata ya Mkata alipokuwa akipita kuelekea Tanga mjini kwenye ufunguzi wa Bomba la Mafuta.
Magufuli amesema kuwa uchunguzi ufanyike Haraka iwezekanavyo ili fedha nyingine Milioni 800 zilizotenga kwaajili ya kumalizia jengo hilo la Hospitali ziletwe na kufanyiwa kazi iliyokusudiwa.
Amesema kuwa ataendelea kutumbua majipu hususani kwa wale ambao wamezoea kuiba fedha za miradi ya wananchi hususani wannchi wanyonge na kwamba anataka watanzania wanyonge waweze kuifurahia nchi yao.
“Siku 15 jibu liwe limepatikana ili fedha nyingine zije, kama kuna mkandarasi hafai afukuzwe au mtu mwingine yeyote hafai aondolewe ili tuanze ukurasa mpya , Mkuu wa Wilaya simamia hili kwa sababu lipo ndani ya uwezo wako”amesema Magufuli
.
Aidha Mh.Rais Magufuli amesema kuwa kuhusu suala la maji Serikali imeanza kushughulikia likiongozwa na wabunge wa majimbo ya Handeni, kiasi cha Bilioni 2 zimetolewa ili kuhakikisha kwamba tatizo la maji linakwisha na atahakikisha Mkata na Handeni wanaondokana na tatizo hilo.
Sambamba na hilo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania leo amewarudishia wananchi wa Kata ya Kabuku ekari 50 za ardhi walizokuwa wamewapa JKT Mgambo zaidi ya miaka 10 kwaajili ya ujenzi wa Kiwanda ambacho hakijaendelezwa, Amewataka JKT kujenga kiwanda ndani ya maeneo yao kwani wanayo maeneo makubwa yenye nafazi za kujenga .
Mh. Raisi amewataka wakazi wa Handeni na Tanga kwa ujumla kujipanga kunufaika na fursa ya bomba la mafuta ili kuinua familia zao kiuchumi kwa kufanya kazi kwa juhudi, kulima mazao ya chakula ya kutosha ,amehakikisha kuwa mradi huu utatoa mchango mkubwa wa kimaendeleo kwa wananchi wa Tanga na Tanzania kwa ujumla.
“ Wananchi na watani zangu Tanga inafunguka kiuchumi, nawahakikishia kwamba mradi huu ni mkubwa na utazidi kuinua uchumi wetu zaidi ya KM1000 zinajengwa ndani ya Nchi ya Tanzania tu, watu watafanya biashara, wananchi watapata vibarua na kazi za kudumu” Amesema Mh. Rais Magufuli.
Mwisho amewataka wananchi wa Tanga kudumisha ummoja na mshikamo kwa kuwatumia vizuri viongozi kwenye kuleta maendeleo na kuwataka vijana kuacha kutumika na watu wasiopenda kuona Tanzania inakuwa na amani, wasidanganywe na vitu vya bure kwani huu ni wakati wa kufanya kazi ili kuweza kupata fedha za halali na kwamba hakuna vitu vya bure.
Mh. Rais Magufuli anatarajiwa kuweka jiwe la Msingi kwenye bomba la Mafuta linalotoka Uganda, Hoima hadi Bandari ya Tanga, Tanzania tarehe 5/8/2017, Viongozi mbalimbali Waziri wa Afya,Ustawi wa jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mh.Ummy Mwalimu, Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh.Januari Makamba,Wabunge wa Handeni, Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Wilaya ya Handeniwalishiriki kwenye mikutano iliyofanyika Kata za Mkata, Komkonga, Kabuku na Segera (Michungwani) Wilayani.
Kwa kwanza kushoto ni Diwani wa Kata ya Mkata akifuatiwa na wakuu wa Idara wa Halmshauri ya Wilaya ya Handeni wakiongoza msafara njiapanda ya Handeni kumpokea Rais.
Viongozi mbalimbali wakiwa tayari kumpokea Rais.
Diwani wa Kata ya Mkata akizungumza shida zake mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Baadhi ya wananchi wliojitokeza kumlaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mbunge wa Handeni Vijijini Mh. Mboni Mhita akizungumza na wananchi wa Mkata.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa