Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw.William Makufwe amewataka walimu,Wakuu wa shule za Sekondari na Walimu Wakuu wa shule za Msingi kufanya kazi kwa Uadilifu,Uaminifu na uwajibikaji ili kukuza taaluma .
Ameyazungumza hayo jana alipokuwa kwenye kikao kazi na walimu wa Kata ya Kwachaga kilichofanyika Shule ya Msingi Taula, chenye lengo la kuinua taalumu kwenye shule za Msingi na Sekondari kwa kujitafakari mahali taalumu ilipotoka, ilipo na inapoelekea .
Mkurugenzi amesema kuwa Serikali imewaamini na kuwapa dhamana waliyonayo hivyo ni vyema kusimamia vyema vizuri majukumu waliyopewa, alisema kuwa walimu lazima wawe na nidhamu ya kazi ili hata wanaofundishwa waweze kupata mifano kutoka kwa walimu wao.
“Walimu lazima muwe na malengo katika kazi zenu mbali na changamoto mbalimbali mazopitia, weledi wa taaluma na malengo yanayofikika , naamini walimu mnao uwezo wa kufanya taaluma ipande au ishuke”. Alisema Makufwe.
Aidha aliwataka wakuu wa shule na walimu wakuu ambao ni wajumbe kamili kwenye vikao vya maendeleo vya Vijiji(KAMAKA) kupeleka matokeo ya wanafunzi na kuweka agenda ya kuinua taaluma kwa wananchi kama agenda ya kudumu itakayojadiliwa na wananchi wote ili kujitathmini kwa pamoja na kuona maendeleo ya watoto wao hatimaye kurahisisha ushiriki wa jamii kwenye kuinua elimu na taaluma kwa ujumla.
“walimu mpeleke ripoti za watoro,matokeo ya majaribio na kitaifa na taarifa za maendeleo za shule za Msingi na Sekondari, taaluma izoeleke kama moja ya maendeleo kwa jamii na wazazi/walezi watatambua wajibu wao” alisema Makufwe .
Katika kuhakikisha watoto wanapata chakula shuleni Mkurugenzi ameataka walimu kuwashirikisha wanafunzi kwenye elimu ya kujitegemea (EK) kwa kulima walau ekari 2 za mazao ya mahindi, maharage na mbaazi , lengo likiwa ni kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula bila bugudha yoyote.
Wakati huohuo Mkurugenzi amewataka walimu kufuata miongozo na kuzingatia matumizi sahihi ya fedha za Serikali zinazoletwa kwaajili ya maendeleo ya shule na kusema kuwa marufuku kubadili matumizi ya fedha na kwamba hatakuwa tayari kumvumilia yeyote atakayekwenda kinyume na maelekezo.
Mkurugenzi alisema ataingia mkataba na Maafisa elimu yenye lengo la kuongeza ufaulu kwa 30% na Maafisa elimu wataingia makubaliano na walimu katika kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa yanafikiwa.
Ziara ya kikazi ya Mkurugenzi Mtendaji na walimu, wakuu wa shule na walimu wakuu kwa Kila kata imenza jana na itaendelea kwa kata zote 21 katika kuhakikisha malengo ya;iyowekwa yanafikiwa na changamoto wazokabili walimu zinazoweza kutatuliwa na ofisi ya mkurugenzi zinatatuliwa kwa wakati.
Matokeo ya darasa la saba Halmshauri ya Wilaya ya Handeni imepanda kutoka 62.3% mwaka 2016 hadi 72.55% mwaka 2017 ambapo kitaifa imeshika nafasi ya 83 Kitaifa kati ya Halmashauri 186 na nafasi ya 5 kimkoa kati ya Halmashauri 12.
Matokeo ya kidato cha nne Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imepanda kutoka 66% mwaka 2016 hadi kufikia 76% mwaka 2017 ambapo kimkoa imeshika nafasi ya 8 kati ya Halmashauri 12 na Kitaifa nafasi ya 155 kati ya Halmashauri 195.
Mkurugenzi Mtendaji Bw. William Makufwe akiendelea kuzungumza na Walimu kwenye darasa la shule ya Msingi Tuliani.
baadhi ya waalimu
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kwachaga Bi. Halima Salim akielezea changamoto zinazoikabili shule yake na namna wanavyojipanga kuboresha taaluma.
Mkuu wa shule ya Sekondari Kwachaga Bw.Halid Ibrahimu akielezea changamoto za shule yake kwa Mkurugeni na Maafisa Elimu.
Walimu wakisikiliza kwa makini maelekezo kutoka kwa mKurugenzi Mtendaji.
Mwalimu wa masomo ya Science shule ya Sekondari Kwachaga Bw. Jacob Onesmo akieleza changamoto anazopitia ili kupatiwa ufumbuzi.
Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Fikeni Senzighe akifafanua baadhi ya maswali waliyouliza walimu waliyouliza kwenye kipindi cha kusikiliza kero zao na changamoto
Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw.Simoni Mdaki akifafanua maswali ya walimu waliyouliza ili kujua mustakabari wao.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa