Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni Bw. Saitoti Zelothe Stephen amekutana na kufanya kikao na wadau wa zao la Muhogo kwenye Halmashauri ya Handeni.
Wadau hao ni pamoja na Wakulima wa zao la Muhogo, Banki ya NMB, Taasisi ya utafiti wa mazao jamii ya mizizi kutoka Kibaha (TARI), Taasisi inayosimamia mnyororo wa thamani wa uzalishaji na usambazaji wa mbegu bora za muhogo (MEDA), Taasisi ya Kilimo ya Kitaifa katika ukanda wa joto (IITA) na Kampuni ya Kibiashara ya kununua muhogo na kusafirisha nje ya nchi (Dar Kanton).
Bw. Saitoti amesema biashara ya muhogo inahitaji uadilifu na uaminifu wa kila mtu kwa uapnde wake na Halmashauri inajukumu la kuhakikisha zao la muhogo liwe na manufaa kwa Halmshauri na kwa kila mkulima mmoja mmoja.
Kwa kumalizia Mkurugenzi Mtendaji Bw. Saitoti Zelothe Stephen ametoa maelekezo kwa wataalam wa sekta ya kilimo kwenda kwa wakulima kutoa elimu ya namna ya uchakataji wa muhogo kuanzia Jumamaosi ya tarehe 09/10/2021 ili kuongeza thamani kwaajili ya kupata faida na kurejesha marejesho.
Afisa kilimo Wa Halmashauri ya Handeni Ndugu Yibalila Kamele Chiza amesema muhogo ni zao moja wapo la kimkakati kwenye Halmashauri ya Handeni hivyo Halmashauri iliamua kutafuta mkopo ili kuwakopesha wakulima na vikundi 43 vya wakulima wa muhogo wenye watu zadi ya mia saba wamepata mkopo wa kilimo cha muhogo kwenye Halmshauri ya Handeni, sasa wanatarajia kuvuna na kuuza hivyo kubadilisha maisha ya wananchi wa Handeni kwa kuongeza kipato chao.
Kwa upande wa Meneja wa banki ya NMB Handeni Bw. Kilonzo amesema wao ni wadau wa kilimo cha muhogo na walishatoa mkopo kwa wakulima wa Handeni kiasi cha Bilioni 3.4 sasa wanatoa fedha kwaajili ya kuandaa vifaa vya kukaushia muhogo ili wakulima kuongeza thamani ya mazao yao kwaajili ya kupata faida na kurejesha marejesho.
Mnunuzi wa Muhogo kutoka Kampuni ya Kibiashara ya kununua muhogo na kusafirisha nje ya nchi (Dar Kanton) amesema kuwa wako tayari kununua muhogo mkavu kutoka kwa wakulima wa muhogo wa Handeni na muhogo unaochakatwa na maganda yake unahifadhika kwa muda mrefu.
Pia amesema wataleta mashine kumi na tano za kuchakatia ili wakulima waweze kuchakata muhogo kwa haraka na watanunua muhogo kwa ujazo wa kilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni Bw. Saitoti Zelothe Stephen, akiwasikiliza kwa makini wakulima wa muhogo.
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Handeni Ndugu.Yibalila Kamele Chiza akisoma taarifa ya zao la Muhogo kwenye Halmashauri.
Afisa Utumishi Bw. Maximillian Makota akiongea kwenye kikoa hicho.
Maafisa Mapato na Biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni wakisikiliza maagizo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo.
Wadau wa zao la Muhogo kutoka benki ya NMB.
Mnunuzi wa Muhogo kutoka kampuni ya Dar kantoni, akieleza jambo kwenye kikao hicho.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa