Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Saitoti Zelothe Stephen amefungua semina ya ya ufuatiliaji na udhibiti wa matumizi ya dawa kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya na namna ya uagizaji wa dawa kutoka Bohari kuu ya dawa.
Bw. Stephen amempongeza na kumshukuru Mhe Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuiona sekta ya afya kwa unyeti wake na kuamua kutoa kiasi cha Milioni 250 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Sindeni kwenye Halmashauri yetu ya Handeni.
Pia Mkurugenzi Mtendaji amewapongeza sekta ya Afya kwa utendaji wao wa kazi lakini amewakumbusha kufanya kazi kwa bidii na kila mmoja aipende kazi yake na atimize majukumu ya kwenye idara. Semina hii imekuja Handeni kwakuwa kuna watu hawatimizi wajibu wao ndiyo maana wawezeshaji wamekuja kuwakumbusha ili mtimize wajibu wenu.Ameeleza.
Ameongezea kusema kuwa kama Halmshauri hatuwezi kutumia fedha kwaajili ya kutoa elimu kwa watu ambao tayari wameshasomea ujuzi huo yatuapasa kutumia lasilimali fedha kwaajili ya kutolea huduma kwa jamii. Lengo la semina hii ni kupata matokeo chanya ya mapato na upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma.
Kwa kumalizia Bw. Saitoti Z. Stephen amewaongoza timu ya usimamaizi ya afya kuweka maazimio ambayo yatawaongoza kusimaia na kuleta ufanisi wa kazi kwenye utendaji wa kazi.Maazimio hayo ni
1: Timu ya usimamizi wa afya kupitia taarifa ya uagizaji dawa.
2: Ujazaji wa fomu za bima ya afya ufanyike kikamilifu na kwa usahihi na kuata mrejesho wa fedha zilizokatwa.
3: Taarifa za uagizaji dawa kutoka kwenye vituo vya kutolea huduma, zifike kwa mfamasia kabla ya tarehe nne ya kila mwezi.
Nao wawezeshaji wa semina hii wamempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni kwa kuamua kuweka utaratibu wa kila mkuu wa idara kuwa mlezi wa kata ili kurahisisha ufuatiliaji wa maendeleo ya kata pamoja na swala zima la afya kwa kila kata kwa ukaribu zaidi.
Kwa upande wa kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri Dkt. William Awe amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji kwa kuandaa semina hii ili kuwakumbusha wataalam majukumu yao ili walete matokeo chanya ya mapato na upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya. Na swala la msamaha tumepata elimu ya kutosha kuahidi kuyafanyia kazi.
Afisa ustawi wa Jamii Ndugu Jovin John ameeleza kuwa kundi la watu maalum ndiyo wanaopaswa kupewa msamaha na sio kila mtu, ameyataja makundi hayo ni pamoja na watu wanaopata ajali wanaenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya wakiwa na fomu ya polisi namba tatu, wazee wasiojiweza, watoto chini ya miaka mitano wakiwa na kadi za kliniki pamoja na wamama wajawazito hivyo amewakumbusha wakuu wa vituo vya kutolea huduma za afya wanapotoa msamaha waangalie kundi hilo lenye uhitaji kulingana na miongozo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni Bw. Saitoti Z. Stephen akiongea wakati wa ufunguzi wa Semina hiyo.
Kaimu Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Dkt. William Awe akitoa ufafanuzi kwenye kikoa hiko
Ndugu Vendavenda Sumuni ambaye ni katibu wa Afya akisikiliza kwa umakini maagizo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmahauri.
Afisa Ustawi wa Jamii Ndugu Jovin John aliyesimama akitoa ufafanuzi kwenye kikao hicho.
Baadhi wa wshiriki wa semina hiyo.
Wataalam wa Idara ya Afya wakiwa makini kuwasikiliza wawezeshaji wa Semina hiyo.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa