Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe amezindua kiwanda cha kufyatulia tofali kinachomilikiwa na Halmashauri.
Bw. Makufwe ameishukuru timu ya ushauri ya Halmashauri (Wakuu wa Idara) kwa kuridhia kuanzisha mradi wa kufyatua tofali na amesema mradi huo utaleta faida kwenye Halmashauri kwani wateja wapo tayari wanasubiria huduma ya upatikanaji wa matofari hayo, hivyo amehimiza uzalishaji uwe mkubwa ili Halmashauri iweze kupata faida kwa haraka.
Kwakumalizia Mkurugenzi Mtendaji Bw. William Makufwe amesema Halmashauri imejipanga kuanzisha miradi yake kwaajili ya kujiongezea kipato kwakupitia makusanyo yake ya ndani. “Baada ya kiwanda cha kufyatulia matofali Halmashauri itanzisha kiwanda cha kupasua mawe na kokoto katika kijiji cha Mazingara hivyo kuongeza wigo wa makusanyo ya mapato” alisema na kutoa wito kwa watumishi wote wa Halmashauri kuilinda na kuitunza miradi hiyo.
Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bi. Edina Katalaiya amesema kiasi cha Milioni 31 zimetumika kwaajili ya kugharamia mradi huo wa kufyatulia matofali. Gharama hizo ni pamoja na ununuzi wa mashine, kujenga kibanda cha kuwekea mashine, kuweka umeme wa njia tatu na kuweka maji.
Bi Edina amesema matofali hayo ni kwaajili ya kuuza kwa kila mtu binafsi na taasisi za Serikali na kuongeza kusema kuwa kutakuwa na matofali yenye viwango tofauti na kila tofari moja litauzwa kuanzia shilingi 1000 hadi shilingi 1800 kutokana na mahitaji ya mteja.
Mwenyekiti wa kamati ya fedha, uchumi na mipango pia ndiye mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Mussa Mwanyumbu wa kwanza kushoto, akiongoza kamati hiyo kutembelea kiwanda cha kufyatulia tofali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni Bw. William Makufwe aliyeshika chepe, akiweka mchanga kwenye mashine ya kufyatulia tofali.
Mkuu wa idara ya utumishi Bw. Charles Mwaitege, aliyeshika chepe akiweka mchanga kwenye mashine ya kufyatulia tofali.
Afisa Mipango wa Halmashauri ya Handeni Bi. Edina Katalaiya aliyeshika kitabu, akitoa ufafanuzi wa mradi huo.
Wakuu wa Idara na vitengo wakimsikiliza Mkurugenzi wakati wa uzinduzi huo.
Muonekano wa matofali yaliyofyatuliwa baadaya uzinduzi wa kiwanda.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa