Aliyasema hayo jana katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika Kata ya Komkonga Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga.
Bw.William Makufwe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alisema jamii ikishirikiana itatokomesha ukatili wa kijinsia ikiwepo mfumo dume na ubakaji.
Pia ameitaka jamii kupiga vita mimba na ndoa za utotoni ili vijana wa kike washiriki katika shughuli za maendeleo na kufikia ndoto zao kiuchumi.
Aidha amesema jamii kuhakikisha wanasimamia haki ya elimu kwa mtoto wa kike kwasababu baadhi ya wazazi huwapeleka vijana wa kiume shule na kuwaacha wa kike nyuma kitu kinachowapelekea kufikia ndoto zao kielimu.
Alitimisha kwa kuwaasa wananchi kuwa makini kwa kuwa ugonjwa korona unazidi kusambaa katika nchi za Afrika
Pia alishukuru wahisani wa shirika la Tanzacare na CAMFED kwa kusaidia kufanikisha maadhimisho hayo
Katika maadhimisho hayo pia vikundi vya kina mama, vijana na walemavu walipewa mkopo jumla ya kiasi cha Shilingi milioni 20 kutoka asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo mkopo huo unatolewa bila riba.
Akisoma taarifa kwa niaba ya wanawake Bi.Kijali amesema wanawake wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazowarudisha nyuma kimaendeleo ikiwepo mfumo dume katika familia hasa katika masuala ya kiuchumi, riba kubwa za mikopo zinazotozwa na taasisi za fedha na uhaba wa maji unaopelekea wanawake kutokufanya dhughuli za uzalishaji badala yake kwenda kutafuta maji.
Maadhimisho ya siku ya wanawake hufanyika kila mwaka kila ifikapo tarehe 8.03 ambapo mwaka huu yalikuwa na kauli mbiu inayosema "KIAZAZI CHA USAWA KWA MAENDELEO YA TANZANIA YA SASA NA YA BAADAYE".
MWUSHO
Imeandaliwa na;
Paulina John
Kitengo cha Habari na mawasiliano Handeni DC
Mgeni rasmi ambaye pia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw.william Makufwe akizungumza na wananchi wa Kata ya Komkonga
Mwakilishi wa wanawake Bi.Kijali akisoma taarifa
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii Bi.Rachel Mbelwa akizungumza
Katibu Tarafa ya Mzundu Bi.Elizabeth akifanya utambulisho wa Viongozi
Mgeni rasmi Bw.William Makufwe akikagua bidhaa zilizoletwa katika siku ya maadhimisho ya wanawake
Mgeni rasmi Bw.william Makufwe akitoa mikopo ya bila riba kwa vikundi vilivyokidhi vigezo.
Mwakilishi wa Umoja wa Wanawake Mkoa akitoa neno la nasaha
Mgeni rasmi Bw.william Makufwe akimkabidhi taulo za kike zilizotolewa na shirika la CAMFED Mtendaji wa Kata ya Komkonga kwaajili ya kugawa kwa wanafunzi wa kike shuleni
Burudani mbalimbali zilikuwepo
wananchi walijitokeza kwa wingi kuadhimisha siku ya wanawake
Diwani wa Tarafa ya Mzundu Mh.Sophia Sowa akikata keki ya siku ya wanawake
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa