Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe ameipongeza serilikali ya awamu ya tano kwa kuleta amani na utulivu kwa Taifa, ameyasema hayo kwenye madhimisho ya siku ya wanawake duniani yanayoadhimishwa kila tarehe 8 machi na yaliadhimishwa kiwilaya kwenye kata ya Mazingara. Kaulimbiu ya mwaka huu ni Wanawake katika uongozi ni chachu ya kufikia usawa wa kijinsia.
Bw. Makufwe amesema mwanamke akipewa uongozi anafanya vizuri na anakuwa kiongozi bora, hivyo amewaasa wazazi wapeleke watoto wao wa kike shuleni kwani elimu ni bure na ukimsomesha mototo wa kike jua umesomesha Taifa na akitolea mfano wa makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambaye ni mwanamke na kiongozi bora kwewnye taifa la Tanzani.
Kwa Halmashauri ya wilaya ya Handeni asilimia nne ya mapato ya ndani yanaenda kwa kinamama kwaajili ya kuanzisha vikundi na Handeni ni Halmashauri pekee ya Mkoa wa Tanga ambayo imeweza kujenga kiwanda kinachomilikiwa na kinamama cha kuchakata muhogo ili kujikwamua na umasikini na utegemezi.
Kwakumalizia Mkurugenzi Mtendaji amesema kuwa kwenye jamii bado kunachanagamoto za ukatili wa kijinsia na watoto wa kike wananyanyaswa na hawapelekwi shule ametoa rai kuwa wazazi wote wasiowapeleka watoto wao shule wakamatwe na wapelekwe polisi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni Bw. William Makufwe aliyevaa suti akimpa zawadi ya pesa na sabuni mama ambaye ni mlemavu wa macho kwenye maadhimisho hayo.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii Bi. Rachel Mbelwa wanne kutoka kulia akiwa pamoja na kikundi cha kinamama cha Mazingara.
Kikundi cha kinamama cha Segera wakionesha bidhaa zao kwenye maadhimisho hayo.
Kinamama wakisonga ugali kwaajili ya kuuza ili kujiongezea kipato kwenye maadhimisho hayo.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa