Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe amefanya kikao cha hadhara na wananchi wa kijiji cha Taula kilichopo kata ya Kwedizinga ili kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.
Bw. Makufwe amewashukuru wananchi wa kijiji cha Taula kwa kujitokeza na amewapa nafasi ya kueleza kero mbalimbali zinazowasibu kwenye kijiji chao kisha kuzitolea ufafanuzi. Akijibu na kuzitolea ufafanuzi kero za wananchi Mkurugenzi amesema Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imepeleka kiasi cha milioni sitini (Tsh.60M) shule ya sekondari Kwedizinga kwaajili ya ujenzi wa madarasa na miundombinu ya shule, pia imepeleka milioni arobaini na saba (Tsh.47M) kwaajili ya ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo kwenye shule ya msingi Taula na kiasi cha milioni arobaini na saba (Tsh.47M) kwaajili ya ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo kwenye shule ya msingi Ugweno.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni amesema kuwa za zahanati ya Taula itafunguliwa tarehe 26/08/2020 kwa kuwahudumia wananchi wa Taula na Handeni kwaujumla ameongezea kueleza kuwa hivi karibuni Halamshauri inatarajia kufungua zahanati ya Nkale iliyopo kata ya Kwamatuku, zahanati ya Kwamsangazi iliyopo kata ya Kwankonje na zahati ya Kwedikwazu iliyopo kata ya kwedikwazu ili ziweze kutoa huduma kwa jamii.
Kwakumalizia Bw. Makufwe amesema kuwa viongozi kwenye Halmashauri yake waandae misaragambo ya miradi ya maendeleo na wampe taarifa atashiriki shughuli za maendeleo kwa vitendo kwa kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoka ofisini kwenda kushiriki shughuli za maendeleo kwa jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bw. Wiliam Makufwe wa pili kushoto akisikiliza kero kutoka kwa mwananchi wa Kijiji cha Taula.
Mkurugenzi mtendaji Bw. Makufwe kushoto akitoa maelekezo kwa mwenyekiti wa kijiji cha Taula wakati akikagua jengo la zahanati ya Taula.
Afisa Utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bw. Charles Mwaitege aliyevaa shati jeupe akisikiliza kero kutoka kwa wananchi.
Afisa mifugo wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bw. Sekiara N. Kiariro aliyeshika maiki akitoa ufafanuzi kwenye kikao hicho.
Wananchi waliojitokeza kumsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni na kutoa kero zao.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa