Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw,William Makufwe awashukuru BAY PORT Taasisi ya kifedha kwa msaada wa kompyuta mbili walizozitoa Jana kwa Idara ya Utumishi na Rasilimali watu.
Mkurugenzi Mtendaji alisema kuwa anashukuru kwa msaada wa kumpyuta hizo ambazo zitakwenda kwenye Idara ya Utumishi na Rasilimali watu ili kuimarisha Idara na ufanisi wa Idara hiyo kwa kuzingatia unyeti wa eneo hilo na huduma wanayoitoa kwa watumishi.
Aliongeza kuwa, Miongoni mwa Halmashauri 80 ambazo zimelenga kufikiwa na BAYPORT tunashukuru Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imekuwa moja wapo na tunaahidi kutumia vifaa hivi vya TEHAMA kwa kuongeza ufanisi na utendaji kazi ulioboreka zaidi.
Mratibu wa masoko na mawasiliano wa huduma za kifedha za BAYPORT Bi.Mercy Ndunguru alisema kuwa BAYPORT imeamua kurudisha faida ambayo wameipata ambapo kwa sasa wameona waguse sekta ya utumishi ambayo imekuwa na msaada mkubwa katika kufikia malengo.
Mercy alisema kuwa, Tunaamini kwa kutoa vifaa hivi vya TEHAMA itasaidia kuongeza ufanisi kwenye sekta ya utumishi na watumishi watapata huduma kwa wakati, BAYPORT inamuunga mkono Raisi kwenye utendaji kazi kwa watumishi.
Meneja wa BAYPORT Handeni Bi. Kanji Masanji alisema kuwa, anashukuru kwa ushirikiano anaoupata kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na kwamba taasisi yao inajipanga kufanya mambo mengine makubwa zaidi ya haya ikiwa ni pamoja na kujipanga kufadhili timu mbalimbali za mipira na kuinua vipaji vya vijana waliopo Wilayani Handeni.
BAYPORT wametoa msaada huo wa kompyuta mbili ikiwa ni miongoni mwa kompyuta zenye thamani ya zaidi ya milioni 500 zinazoendelea kutolewa kwenye taasisi nyingine za Kiserikali.
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano ambapo kushoto ni Mkuu wa Idara ya Utumishi na Mkurugenzi Mtendaji na kulia ni mratibu wa masoko na mawasiliano na meneja wa tawi la BAYPORT Handeni.
Mkurugenzi Mtendaji Bw. William Makufwe kushoto akipokea msaada wa kompyuta kutoka kwa mratibu wa masoko na mawasiliano BAYPORT Bi. Mercy Ndunguru
Mkuu wa Idara ya Utumsihi Bw. Noel Abel akipokea msaada wa kompyuta kutoka kwa mratibu wa masoko na mawasiliano Bi. Mercy Ndunguru.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa