• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Handeni District Council
Handeni District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na Vijana
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Mazingira na Udhibiti taka ngumu
    • Vitengo
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ardhi na Maliasili
    • Kilimo Umwagiliaji na Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Utamaduni na Utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
    • Kilimo
    • Elimu
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maendeleo ya Jamii
      • Kamati ya UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Mfuko wa Jimbo
    • Ratiba ya vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Jarida la Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MKUU WA MKOA WA TANGA AFUNGA MAFUNZO YA KIJESHI YA AWALI KWA VIJANA WA OPERASHENI MAGUFULI AWAMU YA PILI JKT MGAMBO WILAYANI HANDENI

Imerushwa: June 21st, 2017

Mkuu wa mkoa wa Tanga Mh.Martine Shigella amewataka wahitimu wa mafunzo  ya awali ya kijeshi ya vijana operasheni Magufuli awamu ya pili wa kujitolea kutumia mafunzo waliyoyapata kwa kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa niaba ya Taifa la Tanzania.

Hayo ameyazungumza wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya kumaliza mafunzo ya awali ya kijeshi ya vijana operesheni Magufuli awamu ya pili  wa kujitolea yaliyofanyika kwenye  Kituo namba  835KJ Mgambo JKT  kilichopo Kata ya Kabuku Wilayani Handeni.

Mkuu wa Mkoa amesema kuwa mafunzo ya ukakamavu wa mwili, uzalishaji mali, masuala mazima ya ulinzi na usalama na mafunzo ya kijeshi yatumike kwa uzalendo na kuwa mfano bora kwa jamii itanayowazunguka.

“ Nendeni mkawe mfano bora wa kuigwa  kwenye familia zenu na wazazi wenu wamekuja hapa kuwashuhudia, Sisi kama Serikali tunawaamini” alisema Shigella.

Ameongeza kuwa Mh. Rais alipoamua kurudisha mafunzo haya alitambua umuhimu mkubwa kwa Taifa letu sababu anajua mahitaji ya sasa na ya baadae wakati lengo kuu likiwa ni kuleta usawa na uzalendo kwa wasomi na wasio wasomi.

Amewataka wakatimize wajibu wao wa kuwa raia wema na kuwa walinzi wa Taifa kwa kupitia mafunzo ya ulinzi na usalama waliyoyapata huku akieleza kuwa Serikali inapambana na changamoto za kukabiliana na wahalifu  ambao hawataki kuwa kama wanadamu wengine.

 “ Nina imani kubwa na nyinyi kwamba mtaendelea kuwa waadilifu, waaminifu na kuendelea kupiga vita vitendo vya rushwa na ubadhilifu wa mali za umma na kwamba mtakuwa kimbilio la wanyonge na watu wenye matatizo makubwa” alisema Shigella.

Amewasisitiza kuendelea kujiendeleza kielimu ili waweze kupata ajira zinazolingana na hadhi zao. Waje wafanye kazi kwenye viwanda na kwamba rasilimali watu isitegemewe kutoka nje ya Tanga na Tanzania.

Ameeleza kuwa watakaofanya kazi kwenye viwanda watoke Tanzania kwa maana Tanga kuna viwanda vingi vinatarajiwa kuwepo na hivyo nguvu kazi itahitajika ya kutosha na angependezwa kuona miongoni mwao wanatoka JKT Mgambo.

Mwisho amewataka wahitimu kuongeza jitihada za uzalishaji mali hasa kwa kipindi hiki tunchoendea kua Tanzania ya Viwanda  kwani  ili Viwanda viwe na thamani,  wasomi na upatikanaji wa bidhaa zitakazohitajika viwandani hazinabudi kuwepo wakati wote na kwa wingi.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kutenga muda wake kuweza kujumuika pamoja katika kufunga mafunzo hayo. Ameeleza kuwa kuhusu suala la maji atalishughulikia kwa pamoja na Viongozi wa Halmashauri na kwamba atahakikisha maji yanafika Wilayani Handeni .

 Mafunzo ya awali ya Kijeshi kwa Vijana wa kujitolea Operesheni Magufuli yalifunguliwa tarehe 2Jan 2017 yakiwa na jumla ya Vijana 1083 kati yao wasichana 270 na wavulana 813 idadi ya vijana 5 hawakuweza kumaliza mafunzo  kutokana na kijana 1 kufariki, 3 kutorokaa wenyewe na 1 aliahirisha mafunzo hivyo kufanya idadi kubaki 1078.

Mafunzo waliyoyapata ni  uzalishaji mali, huduma za jamii , michezo, mafunzo ya kijeshi ya (Ulinzi na usalama wa Taifa na mafunzo ya kijeshi ya mbinu za kivita,elimu ya mapigano, matumizi ya silaha ndogondogo, usalama na utambuzi, uokoaji, huduma ya kwanza, usomaji ramani, sheria  za kijeshi) n.k.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh.Martine Shigella akitoka kukagua gwaride


gwaride likipita mbele ya mgeni rasmi.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akizungumza na wahitimu.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Kulia akimkaribisha Mkuu wa mkoa wa Tanga kuzungumza na wahitimu.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Martin Shigella akizungumza na wahitimu.

Picha ya pamoja na baadhi ya wakufunzi na Viongozi.

Picha ya pamoja Mkuu wa Mkoa na viongozi mbalimbali.


Baadhi ya wahitimu na viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa.

Tangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO KWA WALIOFAULU USAILI KATIKA NAFASI ZA MWENDESHAJI WA KIFAA CHA BAYOMETRIKI NA AFISA MWANDIKISHAJI MSAIDIZI February 20, 2025
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • HANDENI DC IMEFANYA KIKAO CHA BARAZA KWA ROBO YA NNE YA MWAKA 2023/2024

    August 12, 2024
  • WANAWAKE HANDENI WAMPONGEZI DKT. SAMIA

    August 09, 2024
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA

    August 06, 2024
  • KUPITIA MAPATO YA NDANI, HANDENI IMETEKELEZEKA MIRADI KEDEKEDE

    October 23, 2023
  • Angalia zote

Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amalizia ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Kwedikwazu Mashariki.
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TASAF
  • Fursa za Uwekezaji

Kurasa Mashuhuri

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Tume ya Ajira
  • Ikulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa