Baraza la madiwani la Halmashauri ya Handeni limefanya kikao cha ukaguzi ili kujibu hoja za mkaguzi mkuu wa Serikali. Kikao hicho kimeudhuliwa na Mkuu wa mkoa, katibu tawala, mkaguzi mkazi wa mkoa wa Tanga, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Handeni, Mkuu wa wilaya ya Handeni pamoja na kamati ya ulizi na usalama ya wilaya ya Handeni.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Handeni Mh. Mustapha Beleko, amemshukuru mkuu wa mkoa pamoja na viongozi alioambatana nao kutoka mkoani kushiriki kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Handeni. Mh Beleko amesema kuwa baraza la madiwani la Handeni linashirikiana vizuri na viongozi wa mkoa na wilaya na kutimiza ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa maendeleo ya Taifa na Handeni kwaujumla.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Mh. Martine Shigela aliwapongeza baraza la madiwani kwa kazi nzuri wanayofanya na kupokea maelekezo ya serikali na kuipaisha Handeni kimaendeleo. Pia amewapongeza wafanyakazi wa Halmashauri ya Handeni kwa kuitikia maagizo ya Mheshimiwa Rais ya Halmashauri zote zilizokuwa zinakaa mjini kuhama na Handeni imefanya hivyo mara baada ya kupata maagizo hayo.
Mh. Martine Shigela amewapongeza Mkuu wa Wilaya ya Handeni pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Handeni kwa kuhakikisha muhogo unalimwa kwa wingi Handeni na pia wanafunzi wa shule zote wanakula chakula cha mchana kwa kutumia vizuri elimu ya kujitegemea.
Mkuu wa mkoa huyo amewakumbusha madiwani kubuni vyanzo vingi vya mapato ili kuongeza ukusanyaji wa mapato Handeni. Mh. Shigela amewakumbusha watalamu wa ardhi wa Halmashauri kuwa viwanja vipimwe na viuzwe ili Halmashauri kujiongezea mapato kutokana na uuzwaji wa viwanja.
Katibu tawala mkoa wa Tanga Bi Judica Omary amewaeleza baraza la madiwani kuwa mipango inayopangwa kwaajili ya maendeleo ya Halmashauri ifuatiliwe na iwe ya kutekelezeka kwa haraka. Pia amewakumbusha madiwani kuwafuatilia wanafunzi wa kidato cha sita waliotangaziwa kufunguliwa kwa shule wanarudi haraka shuleni kwaajili ya kwenda kujiadaa na mitihani yao.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Handeni Mh. Athumani Malunda amesema ukaguzi wa ndani ufanyike mara kwa mara kabla ya wakaguzi wan je kuja kukagua. Aidha amesema kuwa vikundi vyote vilivyokopeshwa virejeshe pesa ili wengine nao waweze kukopeshwa.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe kwa upande wake amewapongeza madiwani kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kusimamia ujenzi wa madarasa katika kata zao na kuifanaya Halmashauri ya Handeni kuongoza kwenye ujenzi wa maboma kwa mkoa wa Tanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bw. Williamu Makufwe amemshukuru mkuu wa mkoa pamoja na wageni alioambatana nao kwa kushiriki kikao cha baraza la madiwani la Handeni.
Bw. Makufwe alimuahidi mkuu wa mkoa kuwa maelekezo yote yaliyotolewa yatafanyiwa kazi hasa kuangalia vyanzo vipya vya ukusanyaji wa mapato. Pia suala la zao la mkonge amesema Halmashauri itaanzisha vitalu cha miche ya mkonge na kugawa miche hiyo kwenye shule za Halmashauri ya Handeni ili kuunga mkono juhudi za elimu ya kujitegemea hatimaye shule ziongeze mapato.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mh. Mustapha Beleko aliyesimama akifungua kikao na kuwakaribisha wajumbe wa kikao hicho.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Mh. Martine Shigela akifafanua jambo kwenye kikao hicho.
Katibu tawala mkoa wa Tanga Bi. Judica Omary akisisitiza jembo kwenye kikao maalum cha baraza kujadili hoja za mkaguzi.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe akiongea kwenye kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni aliyesimama akitoa ufafanuzi kwenye kikao maalum cha baraza kujadili hoja za mkaguzi wa hesabu za serikali.
Madiwani wa Halmashauri ya Handeni wakiwa kwenye kikao maalum cha kujadili hoja za mkaguzi wa hesabu za serikali.
Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri ya Handeni Bw. Saturine J. Kessy aliyesimama akisoma hoja zilizojitokeza kwenye kikao hicho.
Mkuu wa mkoa Mh. Martine Shigela wa pili kushoto waliokaa akiwa na wafanyakazi wa Halmashauri ya Handeni.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa