Kituo hicho cha kuuza mafuta kinachomilikiwa na Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzani (TPDC) kinachoitwa TANOIL kilichopo michungwani kata ya Segera kimezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Martine Shigela.
Mkuu wa Mkoa amempongeza Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa juhudi kubwa anayoifanya kwa kuleta maendeleo kwa wananchi na namna alivyoweza kuongoza mapambano dhidi ya ugonjwa wa CORONA (COVID 19).
Pia amempongeza Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kurudisha mali za serilaki zilizokuwa zinamilikiwa na watu binafsi na kuwashawishi wawekezaji kujenga bomba la mafuta kutoka Uganda Mpaka Tanga.
Mh. Martine Shigela amesema Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania wamefanya kazi nzuri ya kutafiti, kuchimba na kusambaza gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam na sasa wameanza kutoa gasi kutoka Dar es Salaam kwaajili ya kusambaza mkoa Tanga ili wananchi waweze kuitumia.
Kwakuhitimisha amewakumbusha wafanyakazi wa Serikali na wananchi kwa ujumla kuwapa ushirikiano Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania kutimiza malengo yao kwa wananchi na faida itakayopatikana itarudi kwa jamii kujenga miundombinu mbalimbali.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dr. James Mataragio amemshukuru Mh Rais kwa kuiwezesha TPDC kurejea kufanyakazi kama hapo awali kipindi cha awamu ya kwanza pia amemshukuru mkuu wa mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na TPDC kwenye miradi yake inayoitekeleza mkoa wa Tanga. Amesema kuwa Shirika litasimamaia usambazaji wa wa uhakika wa mafuta na kwamba watajenga matenki makubwa ya kuwehifadhia mafuta maeneo ya Dar es Salaam, Morogoro, Tanga na Makambako ili wafanyabiashara waweze kuchukulia mafuta karibu na mazingira yao na kwa kipindi cha miaka mitano ijayo watajenga vituo 100 vya mafuta nchi nzima ili kupeleka huduma kwa jamii.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Gondwin Gondwe ameshukuru mkuu wa mkoa kwa kuja kwenye halfa hiyo na kumueleza kuwa wananchi wa Misima wameupokea mradi mkubwa wa bomba la mafuta na wamekubali kuupisha uwekezaji wa bomba la mafuta pia amesema wawekezaji waweze kupitia kwa wakurugenzi na kwa katibu tawala ili wananchi waweze kupata matunda ya uwekezaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe amewashukuru TPDC kwa kuja kuwekeza Handeni na ametoa eneo la kujenga sheli nyingine kwa Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania bure katika kata ya Mkata ambako zipo ofisi za makao makuu ya Halmashauri ya Handeni ili wafanyakazi na wananchi wa Handeni waweze kufaidika na uwekezaji huo.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Mh. Martine Shigela akijaza mafuta kwenye gari ishara ya kufungua kituo hiko.
Mh. Martine shingela wa tatu kushoto akimsikiliza mwananchi mara baada ya kufanya uzinduzi.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Gondwin Gondwe aliyeshika maiki akiongea kwenye uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania Dr. James Mataragio aliyeshika maiki akiongea kwenye uzinduzi huo.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Handeni Bw. William Makufwe aliyesimama kushoto akitoa ufafanuzi wa kutoa eneo kwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania bure ili wajenge sheli.
Wananchi waliojitokeza wakimsikiliza mkuu wa mkoa.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa