Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Omary T. Mgumba amefanya kikao na wananchi wa Kijiji cha Msomera kisha kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali kwenye Kijiji hicho.
Baada ya kusikiliza changamoto na kero mbalimbali kutoka kwa wananchi Mkuu wa Mkoa amesema kuwa,eneo la Msomera ni pori tengefu na eneo la serikali hivyo kwa yeyote aliyekuwa anaishi huko yuko kinyume cha sheria na alikuwa ni mvamizi kama wavamizi wengine wa maeneo tuliyotenga.
Mhe. Mgumba amesema kuwa maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya huduma za jamii kama vile barabara,shule au malisho yaendelee kubaki wazi kama yalivyopangwa na amewaomba wananchi waheshimu mipango ya Serikali kuepusha migogoro isiyofaa.
Pia amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Handeni kuwahamisha watu wote waliolima kwenye maeneo ya malisho au barabara kwa kupewa heka tano tano kwa ajili ya kilimo kwenye maeneo yaliyopangwa kwa ajili ya kilimo na kusimamia matumizi bora ya ardhi kama ilivyoelekezwa kisheria.
Katika ziara yake ya kukutana na wanachi wa Kijiji cha Msomera Mkuu wa Mkoa pia alitembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotelezwa ambapo ni pamoja na ujenzi wa kituo cha Afya Msomera, ujenzi wa mnada na Ujenzi wa bwawa la maji linalosimamiwa na wakala wa usambazaji maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) na amehimiza miradi hiyo ikamilike kwa haraka ili iweze kutoa huduma kwa wananchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni Bw. Saitoti Stephen amesema kuwa anawashukuru wananchi wa Msomera kwa kuitikia suala la Eimu mpaka sasa uandikishaji umefikia zaidi ya 100% na changamoto ya umbali wa Kwenda shule kutoka katika kitongoji cha Mkababu Halmashauri imedhamiria kujenga shule ili wanafunzi waweze kupata elimu kwa ukaribu zaidi.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Omary Mgumba, wa pili kushoto aliyeshika karatasi akisikiliza taaarifa ya Kituo cha Afya Msomera kutoka kwa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Handeni Kulia.
Mkuu wa Mkoa akiendelea kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya Msomera.
Katibu tawala Mkoa wa Tanga Bi. Pili Mnyema, aliyesimama akiongea kwenye kikao Hicho.
Afisa Tawala wa Wilaya ya Handeni Bi. Upendo Magashi, aliyesimama akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Handeni akiongea kwenye kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni Bw. Saitoti Stephen akiongea kwa kujibu changamoto za wananchi wa Msomera.
Wakuu wa Idara kutoka Halmashauri ya Handeni wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Wananchi wa Kijiji cha Msomera waliojitokeza kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa