Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Martin Shigella ameipongeza Halmashauri ya Wiaya ya Handeni kwa kuwa na hati safi na kuwataka kufuata kanuni za manunuzi na kuweka kumbukumbu sahihi ili kuepuka kutengeneza hoja zinazoweza kuzuilika.
Ameyazungumza hayo alipokuwa kwenye kikao cha Baraza la Hoja la CAG kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mwishoni mwa wiki .
Mkuu wa Mkoa amesema kuwa manunuzi yote yanayaofanyika yanapaswa kuwa na vielelezo halali ili kuepuka kutengeneza hoja ambazo zingeweza kufutika, hoja ya kukosekana kwa vielelezo Halmashauri ichukue hatua kwa watendaji watakaohusika ambao wanatumia mianya kujinufaisha wenyewe.
Ameongeza kuwa fedha zinazoletwa ni muhimu zikatumika kwa wakati kwani mahitaji ya wananchi ni mengi na makubwa ili kuepuka bakaa, zibaki fedha ambazo hazikuletwa kwa wakati hivyo kuchelesha matumizi yake, fedha ambazo kwa wakati huo ndio Halmashauri imetangaza zabuni na sio sababu ya kushindwa kutumika.
“wekeni utaratibu wa kuhakikisha kila vikao mnavyokaa hususani kamati ya fedha mnajadili kiasi cha fedha kilichopo kila kwenye akaunti ili kujua matumizi yake kuepuka bakaa zinazoweza kuzuilika, wananchi wanahitaji kuhudumiwa kwa fedha hizo zinazoletwa na Serikali” Amesema Shigella.
Amesema kuwa hoja za malipo kwa watumishi hewa zisijirudie kwa kuhakikisha watumishi wote wanaokuja wanahakikiwa na kulipwa fedha kwa uhalali.
Kwa upande mwingine Katibu Tawala Mkoa Bi. Zena Said amesema kuwa fedha za mifuko ya afya CHF na NHIF hazitakiwi kupita mwaka labda ziwe zimechelewa kuletwa.
Madai ya watumishi kutokuwa na uhalisia ameishauri Halmashauri kuhakikisha madai ambayo watumishi wanayadai kwa Serikali kuwa yamethibitishwa uhalali wake na kuonesha ushaidi na kuondoa dhana ya kufikiri Serikali inafedha nyingi kwaajili ya malipo hayo.
Mwenyekiti wa Wilaya ya Handeni Mh. Ramadhani Diliwa ameshukuru Mkuu wa Mkoa na timu nzima kutoka Mkoani kwa kushiriki pamoja na Halmashuri na kuahidi kusimamia utekelezaji maagizo yote yaliyotolewa kuepuka hoja zinazoweza kuepukika.
Mkaguzi wa ndani Bw. Saturine Kessy akiwasilisha hoja wakati wa kikao.
Baaadhi ya Waheshimiwa Madiwani na wataalamu mbalimbali wakisikiliza kwa makini maoni ya CAG
Waheshimiwa Madiwani katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa