Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Siriel Mchembe akabidhi pikipiki mbili kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Pikipikihizo zimetolewa na Serikali kwa ajili ya Maafisa ugani.
Mhe.Mchembe amesema pikipiki hizo zitunzwe na ziende zikafanye Kazi iliyokusudiwana Serikali kwa wananchi Ili kuongeza uzalishaji wa mazao yatokananayo namifugo iwanufaishe wananchi na Serikali.
Pia Mhe. Mchembe ametoa maelekezo kwa Maafisa ugani wote wa Halmshauri ya Handenikuhakikisha wanakusanya mapato yatokanayo na mifugo na pikipiki hizo zitumikena Maafisa ugani kufika kwenye maeneo yenye mifugo kwa wakati na kuthibitimapato.
Kwaupandewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Handeni Bw. Siatoti Zelothe Stephenameishukuru Serikali kwa kutoa pikipiki kwenye Halmashauri ambazozitasaidia Maafisa ugani kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi vizuri kwenyemazingira yao kutokana na changamoto za maeneo yao kwa Maendeleo ya Handeni naTaifa kwaujumla.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Siriel Mchembe (Kulia aliyevaa blauzi ya njano) akitoa maelekezo kwa mkuu wa idara ya mifugo na uvuvi kushoto.
Katibu tawala wa Wilaya ya Handeni Mhe. Mashaka Boniphace Mgeta akijaribu kuendesha pikipiki hizo.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa