Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Albert Msando (Kushoto picha ya kwanza, aliyevaa suti rangi ya kaki) afanya ziara katika vitongoji vya Mkulumilo na Kwedichocho vilivyopo Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa lengo la kukagua maeneo ya hifadhi za misitu ambayo yamevamiwa na wananchi wanaoendesha shughuli za kilimo kinyume na utaratibu.
Mkuu wa Wilaya huyo pia ameongoza zoezi la kuwakamata baadhi ya wananchi wanaojihusisha na uvunaji holela wa mazao ya misitu na kuagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuwa mbao zote zinazokamatwa zitumike kutengeneza madawati na kupaulia vyumba vya madarasa ya shule zinazojengwa kwenye Wilaya ya Handeni.
*Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa ustawi wa viumbe hai na Uchumi wa Taifa*
Handeni tuko tayari kutunza mazingira, kuokoa vyanzo vya maji kwa Ustawi wa viumbe Hai....!!
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa