Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Toba Nguvila amezindua kampeni ya kudhibiti Malaria na kukabidhi vyandarua kwa wananchi wa wilaya ya Handeni pia ameipongeza Serikali kwa kuanzisha mpango wa kudhbiti Malaria na kutoa vyandarua bure kwa wananchi ili kujikinga na mbu waenezao ugonjwa wa Malaria kwani ndiyo ugonjwa unaongoza kwa kuua watu wengi kwenye wilaya ya Handeni.
Mhe. Nguvila amekemea waliopewa vyandarua kwenda kutumia kwa kujikinga na mbu sio kwenda kufugia kuku na kama kunamtu anampango wa kubadilisha matumizi sheria kali zitachukuliwa dhidi yake.
Kwakumalizia mkuu wa wilaya ameahidi kutoa kompyuta 20 kwa shule ya sekondari Ndolwa ili wanafunzi wajifunze kwavitendo.
Kwaupande wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe ameishukuru selikari kwa kuanzisha mpango wa kudhibiti Malaria na kutoa vyandarua bure kwa wananchi.
Bw. Makufwe amesema maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kwa halmashauri ya wilaya ya Handeni bado ni mkubwa kwani kila watu mia moja, watu sitini na mbili wanamaambukizi ya ugonjwa wa Malaria hivyo kupitia mpango huu asilimia tisini na moja (91%) ya wakazi wa Handeni vijijini watapata vyandarua bure kwaajili ya kujikinga na mbu waenezao ugonjwa wa Malaria.
Kwakumalizia Bw. Makufwe amesema kuwa kila watu mia moja watu tisini na moja watapata vyandarua na kuongeza kusema kuwa Handeni tumejipanga kupambana na malaria kwavitendo.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Toba Nguvila aliyesimama, akiongea kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa wilaya ya Handeni Mhe. Nguvila kushoto akimkabidhi vyandarua mwananchi kulia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe aliyevaa shati jeupe akitoa ufafanuzi kwenye uzinduzi huo.
Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Dkt. Ipyana Mwandelile akitoa taarifa ya hali ya ugonjwa wa Malaria kwenye Halmashauri ya Handeni.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi huo.
Vyandarua vilivyotolewa na Selikari vikiwa tayari kwa kutolewa kwa wananchi.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa