Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe amefanya kikao na wafanyakazi na watumishi wa Halmshauri ya Wilaya ya Handeni mwishoni wa wiki iliyopita katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Mkata na kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi hao na namna ya kuzitafutia ufumbuzi wa matatizo hayo. Mkuu wa Wilaya amewashukuru wafanyakazi wote wa Halmashauri kwa umoja na ushirikiano wao katika ufanyaji kazi na kuleta maendeleo kwenye Halmashauri ya Handeni.
Mh. Godwin Gondwe aliwapa nafasi watendaji Kata kueleza namna kila kata ilivyofikia katika ukusanyaji wa mapato na changamoto zinazowatatiza wasifikie asilimia mia moja (100%) kwa kipindi cha Januari mpaka machi na mwitiko wa wananchi wa kujikinga dhidi ya ugonjwa hatari wa Korona (COVID 19).
Watendaji kata hao wamemueleza Mkuu wa Wilaya kuwa changamoto ya mvua na ubovu wa barabara kuwa kikwazo cha kufikia asilimia mia moja (100%) kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi kwenye ukusanyaji wa mapato na mwitiko wa wananchi kuhusu ugonjwa hatari wa Korona ni mzuri kwani wananchi wanachukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.
Mkuu wa Wilaya huyo amepiga marufuku watoto kufanya kazi au biashara kwani wamefunga shule ili kujikinga na ugonjwa wa Korona (COVID 19) sio kwenda kufanaya kazi.
Pia Mh Gondwin Gondwe amewaagiza wakuu wa idara na wafanyakazi wote kusimamia ukusanyaji wa mapato kwa uadilifu na kutokuwa na visingizio katika ukusanyaji wa mapato ili kufikia malengo yaliyowekwa na kwamba utozaji wa faini ufuate tararibu,sheria na kanuni za nchi za ukusanyajiwa mapato pamoja na kuhakikisha wanashughulikia kero za wananchi ili kuzitatua na kero hizo zikishindikana ngazi ya husika zipelekwe hatua inayofuata kwa maandishi kwa mtu anayehusika.
Wakati huo huo Mh.Godwin Gondwe amepokea msaada wa vifaa vya kujikinga na ugonjwa hatari wa Korona (COVID 19) kutoka kwa Bw. na Bi. Omary Ngole vyenye thamani ya shilingi laki nane (800,000), vifaa hivyo ni pamoja na barakoa, sabuni na ndoo za kuwekea maji.
Mh Gondwe amewashukuru Bw. na Bi. Omary Ngole kwa mchango wao wa kuunga juhundi za Rais katika kupambana na ugonjwa hatari wa Korona (COVID 19).
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Handeni Mh. Athumani Malunda amewapongeza Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe na Mkurugenzi Mtendaaji wa Halmshauri ya Handeni Bw. William Makufwe kwa ushirikiano wao mzuri na wafanyakazi na kwa namna wanavyojituma kufanya kazi ili kuleta maendeleo ya Halmashauri ya Handeni vijijini.
Katibu tawala wa Wilaya Mh. Mwl Boniphace Maiga amesema kuwa wafanayakazi ndiyo kiini cha maendeleo ya Halmashuri na Taifa kwa ujumla hivyo amewakumbusha wafanyakazi kufanaya kazi kwa bidii.
Mwl Boniphace Maiga amewakumbusha maafisa ardhi kuhakikisha wanapima maeneo ya taasisi za serikali kama vile shule, zahanati na vituo vya Afya na kuzipatia hati na kuielekeza idara ya ujenzi kuchore michoro ya majengo ya taasisi za Serikali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe amewashukuru wafanyakazi wa Handeni kwa ushirikisno wao na kufanaya kazi kwa bidii na kuipaisha Handeni.
Pia Mkurugenzi amehadi kununua pikipiki katika Kata ya Sindeni kwajili ya kuongeza ukusanyaji wa mapato katika Kata hiyo. Aidha Bw. Makufwe ameahidi kutoa kiasi cha shilingi laki tano kwaajili ya kununua mabati ya vyumba vitatu vya madarasa ya shule ya msingi Luiye yaliyoezuliwa na upepo na kununua ndoo tano za kufanyia usafi kwenye mnada wa kata ya Kiva.
Kwaupande wa wakuu wa idara kwapamoja wamemueleza Mkuu wa Wilaya kuwa kuna changamoto za uhaba wa watumishi kwa kila idara na ubovu wa barabara kwenda kuongea na wananchi na pia wamemuhakikishia mkuu wa wilaya kuwa wataendelea kutoa elimu dhidi ya ugonjwa hatari wa korona (COVID 19) kwa wananchi na kusimamia ukusanyaji wa mapato kwa asimilia mia moja (100%).
MWISHO.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe akizungumza na watumishi
Katibu Tawala Wilaya ya Handeni Mwl. Boniphace Maiga akisisitiza jambo
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Handeni Mh.Athumani Malunda akizungumza na watumishi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe akifafanua jambo.
Watumishi wa Handeni Vijijini wakifuatilia mazungumzo ya kikao
Mkuu wa Wilaya ya Handeni wa kushoto akipokea msaada wa sabuni,vitakasa mikono na barakoa kutoka kwa mdau Bw.Omary wa kulia
Watumishi na viongozi wakipokea barakoa kutoka kwa mdau Bw. Omary Ngole
Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri wakisoma taarifa kwa Mh. Mkuu wa Wilaya
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa