Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe ameita Asasi za kijamii zilizoko Handeni ili kufanya kikao cha pamoja ambaye aliwakilishwa na Bw.William Makufwe Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni jana katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya lengo likiwa ni kujua shughuli wanazofanya ili kuepuka wadau hao kufanya mradi moja katika eneo moja na kuweka maazimio ya pamoja.Mashirika hayo ni AMREF, CAMFED , WORLD VISION , AGPAHI, ICAP, VISION FUND, DSW ,TAWOREK, NUYAMATA na NALIDO ambazo zinahusika nakusaidia pamoja kutoa elimu kwa jamii
Wakati wa ufunguzi wa kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmasahuri ya Wilaya ya Handeni Bw.William Makufwe amesema mashirika hayo yanatakiwa kufanya kazi kwa kushirikiana na Halmashauri kwa kuziripori shughuli wanazofanya pamoja na kwamba kila shirika linaripoti katika maeneo lake ili Halmasahuri inapoandaa ripoti zake iweze kujumuisha taarifa za shughuli hizo kwa pamoja.
Amewaeleza wadau hao kuwa washirikishe Halmashauri mafanikio na changamoto zinazopatikana katika jamii ili tutatue kwa pamoja na mwisho wa siku tutoke kwenye hatua moja kwenda hatua nyingine na kwamba kila moja atoe mawazo yake, Pia amewasihi kuendelea kuisaidia Halmashauri kwa kutoa elimu kwa jamii kutatua matatizo mbalimbali kupitia misaada kutoka kwa wafadhili kwani Halmashauri inaupungufu mkubwa wa rasilimali.
Amehitimisha kwa kuwataka wadau kuweka maazimio ya pamoja baada ya kusahuriana ili kuweza kufanikisha mikakati ya kuitoa jamii kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine, Maazimio hayo ni kuwa shirika la DSW na CAMFED waangalie utaratibu wa kuwasaidia vijana wa kiume wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwawezesha shughuli za kiuchumi kwani mashirika hayo misaada yao imeelekezwa kwa vijana wa kike zaidi.Shirika la WORLD VISION na CAMFED kukaa pamoja na kuona namna ambavyo wanaweza kufanya mafunzo kwa ushirikiano.
Pia amemtaka mwakalishi wa shirika la walemavu kupata taarifa ya walemavu wanaonyanyaswa hasa wanawake waliopewa mimba na kufikisha ofisi ya Mkurugenzi. Amewataka wadau kutoa taarifa zenye takwimu ya kile kilichofanyika na mafaniko kwenye vikao vya wadau.
Ameongeza kuwa Mashirika binafsi yatoe taarifa ya utekelezaji wa shughuli za miradi yao kila baada ya miezi mitatu na Shirika la ICAP kuboresha huduma ya kubadili tabia kwa vijana baada ya kupima magonjwa ya zinaa hasa UKIMWI.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa