Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Toba Nguvila amefanaya ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Handeni. Miradi hiyo ni pamoja na kikundi cha Jipe moyo cha kuchakata muhogo kilichopo kitumbi, mradi wa maji Mkata, ujenzi wa jengo la makao makuu ya Halmashauri, ujenzi wa jengo la hospitali ya wilaya, ujenzi wa zahanati ya Nyasa na mgodi wa madini wa kwandege uliopo kilimamzinga.
Pia amefanaya ukaguzi wa ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Msomela, nyumba ya mwalimu shule ya msingi Kweingoma, kituo cha kuhifadhia maziwa kilichopo Segera, bweni la wanafunzi shule ya sekondari Kisaza, ukarabati wa shule ya msingi Mgambo, shamba la miti la Korogwe fuels, shamba la miti la kwamsundi na mgodi wa madini wa suwa.
Aidha Mkuu wa Wilaya amempongeza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni na watumishi wote wa Halmashauri ya Handeni kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo ya maendeleo na kutatua kero za wananchi.
Wakati wa ziara hiyo Mh. Nguvila amekutana na wafanayakazi na kufanya kikao kazi na watumishi wa ngazi ya kata kwa tarafa zote za Halmashauri ya wilaya ya Handeni, amabazo ni Mazingara, Kwamsisi, Mkumburu, Mzundu, Magamba na Sindeni na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili kwenye utendaji wao wa kazi na kuzitafutia ufumbuzi ili kufanyakazi kwa weledi kwa maendeleo ya Handeni.
Akikagua bwawa la maji la Mkata mkuu wa Wilaya ameagiza ujenzi wa tenki la maji mkata uanze haraka ili wananchi wapate maji ya uhakika na kumuagiza TAKUKURU pamoja na mkaguzi wa ndani kukagua matumizi ya fedha za mradi wa maji pia ameshauri Halmashauri kuwa na mashine ya kufyatulia tofari ili kupunguza gharama za kununua tofari kwenye ujenzi wa jengo la mako makuu ya Halmashauri.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Toba Nguvila amemuagiza meneja wa TANESCO Wilaya ya Handeni apeleka umeme shule ya sekondari Kisaza na kwenye kiwanda cha kuchakata muhogo kilichopo Kitumbi kinachomilikiwa na kikundi cha Jipe moyo.
Akikaguwa jengo la hospitali ya wilaya linaloendelea kujengwa Mhe. Nguvila amesema kuwa kila tarafa kujenga kituo cha afya ili kupeleka huduma ya afya kwa jamii hivyo amewaagiza wananchi kwa kila tarafa kuandaa kamati za ujenzi na ujenzi uanze mara moja.
Mkuu wa wilaya ya Handeni Mhe. Nguvila ameahidi kutoa tofari elfu nne (4,000) kwaajili ya kumalizia ukarabati wa shule ya msingi Mgambo na kumuagiza meneja wa msitu wa Korogwe fuels kubadilisha jina la Korogwe Fuels na kuitwa Handeni fuels kwani msitu upo Handeni wala sio Korogwe.
Kwakumalizia Mhe. Nguvila amemuagiza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri kuwapa motisha watumishi wanaofanya vizuri kwenye sekta zao na amewahasa watumishi wafanye kazi kwa umoja na ushirikiano.
Afisa mipango wa Halmashauri ya Handeni Bi. Edina Katalaiya kwaniaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni amemshukuru Mkuu wa wilaya kwa kufanya ziara ya kukaguwa miradi inayotekelezwa kwenye Halmashauri pia kuongea na wafanyakazi kusikiliza changamoto zao.
Kwakumalizia Bi. Katalaiya amesema kuwa amepokea maelekezo yote na watakaa na wataalam wenzake waweze kuyafanyia kazi ili Halmashauri isonge mbele kimaendeleo.
Mkuu wa wilaya ya Handeni Mhe. Toba Nguvila aliyevaa suti, akiwa na kamati ya ulinzi na usalama akikagua bwawa la maji lililopo mkata.
Katibu tawala wilaya ya Handeni Mhe. Mashaka Mgeta kushoto aliyevaa shati jeupe akitoka kukagua jengo la ofisi ya serikali ya kijiji cha Msomela.
Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bi. Edina Katalaiya akisikiliza maelekezo kutoka kwa mkuu wa Wilaya ya Handeni kwenye ziara hiyo.
Kamati ya ulinzi na usalama wakishirikiana na wakuu wa idara wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni wakisukuma gari ya katibu tawala baada ya kuingia kwenye korongo ndani ya msitu wa Gole wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya.Baadhi ya wafanyakazi wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni wakitoa kero na malalamiko yao kwa mkuu wa Wilaya ya Handeni wakati wa ziara hiyo.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa