Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Siriel Mchembe amekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 31 kwa Halmashauri ya Handeni vilivyotolewa na Shirika la maendeleo la World Vision Tanzania. Vifaa hivyo ni pamoja na vitanda vya kujifungulia, Kiti cha mgonjwa wa meno na mashine za kupima presha.
Mhe. Mchembe amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha wanawake wa Handeni wanajifungua kwenye mazingira salama na kupitia juhudi zake ameanzisha kaulimbiu ya tuwavushe ili kuondoa changamoto zinazowakabili wanawake wakati wa kujifungua na kupitia fedha za tozo zitokanazo na miamala ya simu Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imepokea kiasi cha Milioni miambili na Hamisi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Sindeni na kwasasa kipo Hatua ya upauaji.
Kwa kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani kwa kuweka mazigira mazuri na salama kwenye sekta ya afya, shirika la World Vision Tanzania imetoa vifaa hivyo kwa ajili ya zahanati za Kwamsisi, Kwandugwa, Pozo, Mkalamo na Kwasunga, Mhe. Mchembe amesema.
Kwakumalizia Mkuu wa Wilaya Mhe. Siriel Mchembe amesema serikali inatambua mchango wa shirika la World Vision Tanzania kwani ni wadau wakubwa wa sekta ya afya Handeni.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya ya Wilaya ya Handeni Dkt. Kanansia Michael Shoo amewashukuru shirika la World Vision kwa Mchango wao kwenye sekta ya afya kwa Halamashauri ya Handeni na kueleza kuwa zahanati ya Kwamsisi itaanza kutoa huduma za wagonjwa wa meno na ameahidi kuvitunza vifaa hivyo ili viweze kukidhi mahitaji ya wananchi.
Kwaniaba ya Mkurugenzi Dkt Kanansia ametoa cheti cha maalum cha shukrani kwa shirika la world vision kwa kutambua mchango wao kwenye sekta ya afya wanavyotekeleza kwenye Halmashauri ya Handeni.
Meneja wa World Vision kanda ya Mashariki Bw. Daniel Chuma amesema kuwa shirika lao linaunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha naisha ya wananchi kwa kutoa elimu za kuelimisha jamii kuhusu afya kwa kutumia vikundi mbalimbali vya sauti za umma, kuwapa semina wataam wa afya na kutoa vifaa kwaajili ya zahanzote za tarafa Kwamsisi.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Mchembe aliyevaa kilemba akisalimiana na wananchi wa Kwamsisi.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Siriel Mchembe, aliyevaa miwani akimfariji wagonjwa kwenye zahanati ya Kwamsisi alipoenda kukabidhi vifaa.
Katibu tawala wa Wilaya ya Handeni Mhe. Boniphace Mgeta aliyesimama akisalimia wananchi Wa Kwamsisi wakati wa kukabidhi vifaa.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Handeni Dkt. Kanansia Michael Shoo akitoa ufafanuzi wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba.
Meneja wa shirika la Kiraia la World Vision kanda ya Pwani Bw.Daniel Chuma akitoa ufafaunuzi wa vifaa.
Wataam wa sekta ya afya pamoja na wananchi wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Handeni.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa