Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Toba Nguvila ameahirisha wiki ya unyonyeshaji kwa mkoa wa Tanga iliyofanyika kwenye Halmashauri ya wilaya ya Handeni.
Mh. Nguvila amempongeza Mkurugenzi Mtendaji pamoja na watumishi wote wa Halmashauri kwa juhudi kubwa wanazozifanya kwa kutoa huduma nzuri za lishe pia amewahasa kinamama kunyonyesha watoto wao kwa muda kama taratibu za kiafya zinavyoelekeza wasiwaachishe watoto wafikapo miezi sita na kuanza kuwapa maziwa ya kiwandani.
Kwakumalizia Mkuu wa Wilaya amesema ofisi za serikali na taasisi zote ziwape wafanyakazi wanawake likizo ya uzazi wanapojifungua ili wanyonyeshe watoto wapate afya njema na wanaume wapewe likizo ya siku tatu kumuhudumia mke wake.
Kwaupande wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe amesema kuwa Halamshauri ya wilaya ya Handeni ni ya pili kati ya Halmashuri kumi na moja kwa mkoa wa Tanga na kuwa na 88.18% vya viashiria vya lishe hivyo wataendelea kutoa elimu kwa jamii na kuhimiza wazazi wawape watoto wao lishe bora.
Pia Bw. Makufwe amesema Halmashauri ya Wilaya ya Handeni inawajali watu waishio na Virusi vya UKIMWI na imekuwa Halmashauri ya kwanza kati ya kumi na moja zilizopo mkoa wa Tanga kwa kuwajali na kuwapa elimu nasihi watu waishio na virusi vya UKIMWI.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Toba Nguvila akiahirisha wiki ya unyonyeshaji mkoa wa Tanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe akisoma taarifa ya lishe ya Halmashauri ya Handeni.Wananchi waliojitokeza kwenye zoezi la kuahirisha wiki ya unyonyeshaji mkoa wa Tanga.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa