Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Toba Nguvila amezindua kampeni ya kupiga vita dhidi ya ukeketaji kwa watoto wakike. Akifungua kampeni hiyo Mh. Nguvila amelishukuru shirika la Kimataifa lisilo la Serikali la Amref Afrika kwa kuchagua Handeni na kuja kutoa elimu ya kupiga vita dhidi ya ukeketaji kwa watoto wa kike.
Pia amesema jamii ya Handeni bado inaimani potofu ya kukeketa watoto wakike amewakumbusha jamii isijihusishe na vitendo vya kukeketa watoto wa kike kwani kufanya hivyo ni kumnyima haki zake pamoja na kumfanya asijianini mbele ya jamii, hivyo kumuelimsha mtoto wa kike ni kuelimisha jamii nzima.
Kwa kumalizia amewaomba wafanyakazi wote wa Halmashuari ya Handeni kutoa ushirikiano kwa Shirika la Amref ili waweze kutoa elimu dhidi ya kupiga vita suala zima la ukeketaji kwa mtoto wa kike.
Katibu tawala wa Wilaya ya Handeni Mhe. Mashaka Boniphace Mgeta amemshukuru Mh. Rais kwa kumchagua na kumuamini na kumleta Handeni kushiriki kasi ya mageuzi ya maendeleo kwa nchi yetu, amempongeza Rais kwa kujitofautisha na Marais wa Afrika kwa kupunguza gharama za matumizi na kupeleka fedha kwa jamii zifanye kazi za maendeleo. Hivyo amewaomba wafanyakazi na jamii nzima ya Handeni kushirikiana na kufanya kazi kwa umoja kwani Handeni ni ya kwetu sote na maendeleo ni yetu wote.
Kwaupande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe amemshukuru mkuu wa Wilaya ya Handeni kuzindua kampeni elimisha ya kupiga vita dhidi ya ukeketaji na kueleza changamoto ya uhaba wa watumishi wa afya kuwa kunauhaba wa asilimia 75% na waliokuwepo wanahudumia vituo vya afya viwili na zahanati arobaini na nne. Na kunampango wa kujenga vituo vya afya kwa kila tarafa na zahanati kwenye Halmashauri ya wilaya ya Handeni.
Pia amewapongeza Amref Afrika kwa kuja kutoa elimu ya mapambano dhidi ya ukeketaji kwenye Hamashairi ya Handeni na kuwahakikishia kuwa watumishi wa Halmashauri ya Handeni wako tayari kuupokea mradi na watatoa ushirikiano mzuri.
Naye afisa mradi elimisha awamu ya tatu Bw. Ibrahim Olekinwaa amemshukuru Mkuu wa wilaya na kumwambia kuwa wameamua kuja kutoa elimu Handeni kwani bado jamii ya Handeni wanaendeleza suala zima la ukeketaji kwa watoto wakike.
Ameongeza kusema kuwa wanamshukuru Mkurugenzi Mtendaji waHalmashauri ya Handeni kwa ushirikaino wake pamoja na wafanyakazi wote na wamemuomba awaongezee kata tano ambazo wataenda kutoa elimu dhidi ya ukatili wa kijinsia wa kukeketa watoto wa kike.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Toba Nguvila akifafanua jambo kwenye uzinduzi huo.
Katibu tawala Wilaya ya Handeni Mh.Mashaka Boniphace Mgeta, aliyesimama akiongea mbele ya wajumbe wa mradi (hawapo pichani).
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe aliyesimama akitoa ufafanuzi wa changamoto za sekta ya afya kwenye uzinduzi wa mradi huo.
Dr. Serafina Mkuwa kiongozi wa mradi kutoka Amref-Dar es Salaam.
Afisa mradi elimisha Bw.Ibrahim Olekinwaa akieleza madhara yatokanayo na ukeketaji kwa watoto wa kike.
Katibu wa afya Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bw. Vendavenda Sumuni aliyesimama.
Wajumbe wa mradi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya kwenye uzinduzi wa mradi elimisha.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa