Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Toba Nguvila azindua mpango wa serikali wa kutambua na kuwapa vyeti vya kuzaliwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano na kuipongeza Serikali na Wakala wa usajili, ufilisi na udhamini (RITA) kwa mpango huu wa kusajili na kutoa vyeti kwa watoto walio chini ya miaka mitano bure.
Mh. Nguvila amesema kuwa usajili wa watoto na kuwapa vyeti vya kuzaliwa ni muhimu kwani itasaidia kutambua idadi ya watoto, kubuni na kupanga mipango mbalimbali ya serikali ya maendeleo na mahitaji ya watoto pia husaidia kupata ajira na kuandaa hati za kusafiria.
Amewakumbusha wahusika waweze kutembea nyumba hadi nyumba sio kukaa ofisini tu na kwenda kufanyakazi kwa weledi na kwa kutenda haki pia ameahidi kufuatilia zoezi hili kijiji hadi kijiji ili kuona namna zoezi linavyotekelezwa.
Kwakuhitimisha Mhe. Toba Nguvila ametoa zawadi ya jezi seti mbili na mpira mmoja kwa vijana wa komkonga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto walio chini ya miaka mitano bure kwani upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa ni changamoto kubwa kwasababu ya mfumo na sheria za usajili kupitwa na wakati.
Kwakumalizia Bw. Makufwe amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imepanga kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto walio chini ya miaka mitano kwa asilimia mia moja (100%) na kuhakikisha watumishi walio kwenye zoezi la usajili kutembea nyumba hadi nyumba kwaajili ya kutoa huduma.
Mkuu wa wilaya ya Handeni Mhe. Toba Nguvila aliyesimama akiwasalimia wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi huo.
Mh. Toba Nguvila kulia mweyekofia ya kahawia akikabidhi jezi na mpira kwa mweneyekiti wa kijiji cha Komkonga.
Katibu tawala wa wilaya ya Handeni Mhe. Mashaka Mgeta aliyevaa shati jeupe akiwasalimia wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa mpango huo.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe aliyeshika karatasi akisoma taarifa ya upatikani wa vyeti kwa Halmashauri ya Handeni.Viongozi wa Wilaya wakishiriki kuchenza ngoma ya kizingua. Mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Dkt. Ipyana Mwandelile katikati aliyevaa koti akisikiliza maelekezo ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi huo.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa