• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Handeni District Council
Handeni District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na Vijana
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Mazingira na Udhibiti taka ngumu
    • Vitengo
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ardhi na Maliasili
    • Kilimo Umwagiliaji na Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Utamaduni na Utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
    • Kilimo
    • Elimu
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maendeleo ya Jamii
      • Kamati ya UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Mfuko wa Jimbo
    • Ratiba ya vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Jarida la Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MKUU WA WILAYA YA HANDENI AMEPOKEA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI WA ZAHANATI VYENYE THAMANI YA SH.MILIONI 14.7 NA KUWATAKA VIONGOZI KUTUMIA KWA MALENGO YALIYOKUSUDIWA.

Imerushwa: November 5th, 2017

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe amepokea msaada wa vifaa vya ujenzi wa zahanati wenye thamani ya Shilingi Milioni 14.7 za Kitanzania kutoka Darworth Ltd Mwekezaji wa kiwanda cha usindikaji matunda, kama shukurani baada ya kupewa ardhi yenye ukubwa wa ekari 10 kwaajili ya ujenzi wa kiwanda hicho Kitongoji cha Mkomba katika Kijiji cha Michungwani kilichopo Wilayani Handeni..

 Akizungumza wakati wa mapaokezi ya vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya amewataka Viongozi ngazi ya Kata kuhakikisha wanasimamia  na kutumia vifaa kwa kadri ilivyokusudiwa na kwamba asitokee mtu yeyote kupindisha matumizi au kusimamisha  ujenzi wa zahanati hiyo ambayo itakuwa na manufaa kwa wananchi wote.


 Ameongeza kuwa yote hayo yanafanywa kwaajili ya wananchi wa Handeni na kwamba maendeleo hayana itikadi, hivyo roho ya maendeleo iliyopo waishikilie ili wasonge mbele kwa pamoja kwakuzingatia kuwa wanatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi.

 Gondwe amesema kuwa Mh.Rais ameagiza kuwepo kwa maeneo yanayotengwa rasmi kwaajili ya viwanda , na sisi kama viongozi tumejumuika kwa pamoja kusimamia agizo la Mh.Rais,  kwa Handeni ni wajibu wetu kuhakikisha tunaendelea kutenga maeneo kwaajili ya viwanda kama ambavyo kiwanda hiki kitakavyojengwa.

 “Asitokee mtu akauondoa umoja huu, huu ni mwanzo tu, viongozi tunakazi ya kuhakikisha vifaa hivi vilivyoletwa vinafanye kazi yake na wananchi waone matunda ya rasilimali yao” amesema Gondwe

 Kadhalka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe  ameahidi kusimamia na kuhakikisha vifaa vyote vinatumika ipasavyo na kutoa ushirikiano kwa mwekezaji ili kufikia malengo ya ukamilishaji wa kiwanda  cha kusindika matunda.

 Kwa upande wake mwekezaji John Kessy kutoka kamupni ya Darworth Ltd  amesema kuwa ujenzi wa kiwanda utakuwa si wa manufaa kwa wananchi wa michungwani tu, bali na  hata kwao wawekezaji na ndiomaana wameona vyema kuchangia ujenzi wa zahanati sababu hata wafanyakazi watakaokuwa wanafanya kazi kwenye kiwanda watanufaika na huduma za afya zitakazotolewa hapo.

 Aliongeza kuwa watafurahishwa kama vifaa hivyo vitasaidia kufikia lengo lililokusudiwa  kwakuwa  huo ni mwanzo  na kwamba watendelea kufanya kazi bega kwa bega  kwa kushirikiana na Serikali ili kufikia uchumi wa Tanzania ya Viwanda.

 Mkuu wa Wilaya amepokea vifaa ambavyo ni Mabati (ya geji 28) 200, nondo Tani3,mifuko 200 ya saruji na mabomba lora 3 ambayo yatatumika kusambaza maji kutoka kwenye zahanati hadi kiwandani na kufanya jumla ya Mil.14.7, hatua ya ujenzi kwa sasa ipo kwenye michoro ambapo kiwanda kinatarajiwa kujengwa kuanzia Januari 2018 na  kukamilika Desemba 2018. Mapokezi hayo yalijumuisha viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya Wilaya hadi ya Kata.

Image may contain: 13 people, people smiling, people standing

Image may contain: 7 people, people smiling, people sitting

Image may contain: 8 people, people smiling, people standing

  Image may contain: 1 person

Image may contain: 8 people, people smiling, people standing, crowd and outdoor 









LikeShow More ReactionsCommentShare


Tangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO KWA WALIOFAULU USAILI KATIKA NAFASI ZA MWENDESHAJI WA KIFAA CHA BAYOMETRIKI NA AFISA MWANDIKISHAJI MSAIDIZI February 20, 2025
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • HANDENI DC IMEFANYA KIKAO CHA BARAZA KWA ROBO YA NNE YA MWAKA 2023/2024

    August 12, 2024
  • WANAWAKE HANDENI WAMPONGEZI DKT. SAMIA

    August 09, 2024
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA

    August 06, 2024
  • KUPITIA MAPATO YA NDANI, HANDENI IMETEKELEZEKA MIRADI KEDEKEDE

    October 23, 2023
  • Angalia zote

Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amalizia ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Kwedikwazu Mashariki.
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TASAF
  • Fursa za Uwekezaji

Kurasa Mashuhuri

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Tume ya Ajira
  • Ikulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa