MNADA WA MKATA WAZINDULIWA RASMI
Mnada wa Mkata umezinduliwa rasmi leo baada ya kuacha kufanyakazi kwa muda wa takribani miaka minne kutokana na sababu mbalimbali ikiwepo utozaji ushuru usiohalali kutoka kwa mzabuni aliyepewa zabuni ya kukusanya ushuru katika mnada huo kwa kipindi hicho.
Akizungumza katika uzinduzi huo mgeni rasmi ambaye pia Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe aliwatoa hofu wafanyabiashara kuwa viwanja vya kufanyia biashara zao zitagawiwa bure na kwamba endapo itajulikana kiongozi yoyoyte atachukua fedha ya kugawa eneo la kufanyia biashara atamchukulia hatua kali za kisheria ”hakikisha unapata haki yako bila malipo, haki hainunuliwi”alisema.
Pia amewataka viongozi kuweka mipaka ya eneo la mnada vizuri kuepusha migogoro na wavamiaji wa ardhi ili wananchi wafanye biashara zao katika mazingira salama na wanufaike na eneo hili na Halmashauri pia ipate mapato yatakayotumika kwa maendeleo ya wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni. Aidha amewataka maafisa ardhi na mipango miji kutengeneza mchoro wa eneo la mnada ili paweze kupitika kwa urahisi, Pia ametaka utozaji wa ushuru wa mifugo uwe baada ya mtu kuuza mfugo na kwamba mtu asitozwe ushuru kama hajauza mfugo na kwa upande wa wauza mbogamboga Gondwe aliagiza kuwa wasitozwe ushuru kabisa.
Alihitimisha kwa kwakuwata wananchi kupeleka migogoro yao kila alhamisi ya wiki ambapo watasikilizwa katika ngazi yoyote kuanzia ngazi ya kijiji hadi ngazi ya Wilaya na kwamba wananchi wahakikishe wanaanzia ngazi za chini endapo itashindikana ndiyo aende ngazi ya Wilaya.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe alisema kuwa malengo ya kufufua mnada huu ni kuongeza ajira kwa wananchi wa Mkata na aliwahakikishia wananchia hao kupata maeneo ya kufanya biashara zao halali bure na alisema kwamba sisi tunatekeleza maagizo ya Mh.Raisi ya kutafsiri kwa vitendo fursa zilizopo katika maeneo yetu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
Makufwe alisema kuwa kwa sasa Halmashuri ndiyo inatoza ushuru hivyo tatizo la watu kutozwa ushuru kama hawajauza mifugo yao haitakuwepo tena lakini aliwataka pia wafanya biashara kuwa waaminifu kwenye ulipaji wa ushuru kwani wengine hata kama wameuza wanakwepa kulipa ushuru, alisema kwamba ushuru huo wanaolipa unatumika kufanyia shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni hivyo wakikwepa kulipa watakwamisha maendeleo ya Handeni.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Mkata Bw. Athumani Ndutu akisoma taarifa katika uzinduzi huo alisema mnada wa Mkata ulianza tangu mwaka 2008 ukafanya kazi hadi 2014 lakini sababu zilizosababisha mnada wa Mkata kufa zilikuwa ni mzabuni kutoza ushuru holela na kutoa lugha chafu kwa wafanya biashara na kutokuwepo na vivuko vya mifugo lakini mwezi septemba 2018 timu ya wataalamu iliundwa ili kufufua mnada wa Mkata ambapo walikaa na kujadili sababu zilizosababisha mnada huo kufa ikiwa ni pamoja namna ya utozaji wa ushuru na vivuko vya mifugo ambapo baada ya timu hiyo kutatua matatizo hayo walifanya kikao cha pamoja na wafanyabiashara wakakubaliana kuuanzisha upya mnada huo.
Mwakilishi wa wafugaji Bw. Amosi Kirindio alisema kuwa wao kama wafugaji watahamasishana kuleta mifugo katika mnada wa Mkata na kwamba wamefurahi kurudishwa kwa mnada huo kwani wanaamini utakuwa mnada bora kuliko minada mingine.
Mkurugenzi Mtendaji Bw.William Makufwe akizungumzaWananchi wakijitokeza kwa wingi katika uzinduzi huoMwakilishi wa wafugaji Bw. Amosi Kirindio akizungumzaAfisa Maendeleo ya Jamii Bi.Rachel Mbelwa akihamasisha mnada huo kuendelezwa
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Handeni akitoa neno katika uzinduzi huo
Mh.Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akizungumza katika uzinduzi huo
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa