Mh. Athumani Malunda aliyasema hayo katika zoezi la uapishwaji wa viongozi wa serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni ambao ni Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji, viti maalum na wajumbe mchanganyiko uliofanyika siku tatu kuanzia tarehe 28-30/11/2019 katika Tarafa sita ambazo ni Tarafa ya Mzundu, Mkumburu, Sindeni, Magamba, Mazingara na Kwamsisi
Amesema kiongozi yoyote ambaye hatafuata kanuni taratibu na sharia za uongozi atachukuliwa hatua au kuondolewa katika wadhifa wake hususani migogoro ya ardhi kwamba wasienda kusababisha migogoro ya ardhi lakini waende kusuluhisha tatizo la migogoro ya ardhi katika maeneo yao hasa migogoro kati ya wakulima na wafugaji na mashamba yaliyouzwa kwa njia isiyo halali yarudishwe kwa wananchi ili waweze kunufaika na mashamba hayo.
Aidha ametoa onyo kwa viongozi wanaokunywa pombe kupindukia na kusahau jukumu la kutumikia wananchi kuwa watanyang’awa vyeo vyao pindi watakapogundulika, pia amewaasa kuwa mfano kwa wananchi hivyo kuwataka viongozi hao hadi ifikapo Disemba 30 2019 wawe na Bima ya matibabu iliyoboreshwa (ICHF) pamoja na vyoo bora.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe aliwapongeza viongozi wa Serikali za Mitaa kwa kupita bila kupigwa kupitia CCM lakini pia amewaasa viongozi hao kujitambua nini wanatakiwa kwenda kufanya katika maeneo yao kwaajili ya kuleta maendeleo ya wananchi ikiwepo kuhamasisha kilimo cha mazao mbalimbali hasa mazao yanayostahimili ukame kama mihogo na korosho pamoja na kuhamasisha wananchi kuchangia shughuli za maendeleo hususani elimu na afya, pia aliwaasa kuwatanguliza wananchi badala ya wao kujitanguliza.
Makufwe ameongeza kuwa kipindi walichochaguliwa ni kipindi cha kufanya kazi siyo ubabaishaji hasa suala la uaminifu na kujituma ili kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano. Amesema vijiji havitakiwi kuuza ardhi zaidi ya ekari 50 na wakiuza zaidi ya hapo ni kinyume na taratibu na kwamba watakaofanya hivyo watachukuliwa hatua za sharia
Naye msimamizi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa Bi. Rachel L. Mbelwa amesema uandikishaji wa wapiga kura ulifanyika kwa amani na utulivu ambapo amesema Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imepata nafasi ya pili Kimkoa na kwa upande wagombea amesema Vjiji vyote 91 na Vitongoji vyote 770 wa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) walipita bila kupingwa huku Mkoa wa Tanga kitaifa ukishika nafasi ya Tatu kwa wagombea wa CCM kupita bila kupingwa.
Bi Rachel amesema viongozi wa Serikali za Mitaa Handeni Vijijini walioapishwa ni 2,275 wakiwepo Wenyeviti wa Vijiji, Wenyeviti wa Vitongoji, viongozi wa viti maaalum na wajumbe mchanganyiko.
MWISHO.
Taarifa hii imeandaliwa na:
Paulina John
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Handeni DC.
Mwenyekiti CCM Wilaya ya Handeni Mh.Athumani Malunda akizungumza katika zoezi kauapishwaji wa viongozi wa Serikali za Mitaa
Mkurugenzi Mtendaji Handeni DCBw. William Makufwe akitoa neno kwa viongozi walioapishwa
Msimamizi wa uchaguzi Handeni DC Bi.Rachel Mbelwa akielezea jambo katika zoezi hilo
Mwenyekiti wa Halmashauri Handeni DC Mh. Mustafa Beleko akitoa nasaha kwa viongozi wanoapishwa.
Waheshimiwa Kata mbalimbali za Handeni DC wakitoa pongeza kwa viongozi wa CCM waliopita bila kupingwa
Wataalam wa Iadara mbalimbali za Handeni DC wakitoa mafunzo kwa viongozi walioapishwa
Viongozi wa Serikali za Mitaa Handeni DC waliopita bila kupingwa wakila kiapo
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa