Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Bw. Amon Mpanju ametembelea Kijiji cha Msomera kwa lengo la kufuatilia na kukagua maendeleo ya uboreshaji wa huduma za ustawi wa jamii na kuamsha ari ya jamii katika kushiriki shughuli za maendeleio ya miradi inayotekelezwa na Serikali katika kijij cha Msomera na kuongea na wananchi.
Miradi hiyo iliyotembelewa na Naibu Katibu Mkuu ni pamoja na ujenzi wa kituo cha Afya Msomera, kituo cha polisi Msomera, shule ya Msingi Samia Suluhu Hassan, Shule ya sekon dari Msomera na mradi wa visima vya maji.
Bw. Mpanju amesema kuwa Serikali itaendelea kutoa mikopo kwa makundi mbalimbali kwa wananchi wa Msomera hivyo wao kama wizara watapeleka maafisa maendeleo ya jamii 12 kwenye Halamashuri ya Handeni hususani kwenye Kijiji cha Msomera ili waweze kusaidian na waliopo kutoa elimu ya ujasiliamali kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.
Naibu katibu Mkuu amesisistiza wananchi wa Msomera kuwatoa Watoto wao kwenda shule kwani elimu ndiyo mkombozi wa maendeleo na Serikali inajenga miundombinu bora ya shule ili watoto wa Msomera waende shule.
Ameongeza kusema kuwa Serikali inayonia ya kuhakikisha Msomera inabadirika kwa kuwa na huduma zinzohitaijka na wananchi washirikiane kuwalea watoto kwenye misingi ya maadili bora za mila zetu kwani malezi mazuri yanaanzia nyumbani.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Albert Msando amesema kuwa Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassaniu ni Sikivu kwani yale yote yaliyopangwa kutekelezwa Msomera yametekelezwa kwa wakati na imeshaanza kutoa huduma kwa jamii na kuwa Kijiji cha Mfano.
Mhe. Msando amesema kuwa watatenga maeneo maalum kwa ajili ya kuandaa mashamba darasa ili wananchi wa Msomera waweze kujifunza kwa vitendo na amemuhakikishia naibu katibu Mkuu kuwa Wilaya itasimamaia utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo na kutatua kero pamoja na changamoto zote za wananchi wa Handeni kwa wakati.
Bw. Amon Mpanju Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum
Bw. Amon Mpanju Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, kulia aliyeshika fimbo, akisikiliza taarifa ya ujenzi wa majosho kutoka kwa afisa Mifugo katikati
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Albert Msando
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa