• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Handeni District Council
Handeni District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na Vijana
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Mazingira na Udhibiti taka ngumu
    • Vitengo
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ardhi na Maliasili
    • Kilimo Umwagiliaji na Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Utamaduni na Utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
    • Kilimo
    • Elimu
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maendeleo ya Jamii
      • Kamati ya UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Mfuko wa Jimbo
    • Ratiba ya vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Jarida la Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Naibu waziri aongea na watumishi Handeni.

Imerushwa: November 29th, 2021

Naibu waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe. Deogratius John Ndejembi amefanya kikao na watumishi wa Halmshauri ya Wilaya ya Handeni pamoja na Halmashauri ya Handeni Mji.

Baada ya kusikiliza kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imejipambanua wazi kujadili maslahi ya watumishi ndiyo maana kwa mapenzi yake Rais alielekeza watumishi 180,000 wapandishwe madaraja kutoka idadi ya 90,000 iliyopangwa awali ya kupandisha watumishi huu ni upendo wa Rais wetu ameuonesha kwa watumishi nchi nzima.

Pia Mhe. Deogratius Ndejembi amesema kuwa serikali imetenga ajira za watumishi 34,000 ambazo zinatarajiwa kutangazwa hivi karibuni Serikali itatoa kipaumbele katika kada ya Elimu na Afya kwani Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewekeza fedha nyingi kwenye miundombinu ya madarasa na vituo vya Afya ili kuhakikisha upungufu wa madarasa unaenda kuisha nchini.

Kwa kumalizia naibu waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe. Deogratius John Ndejembi amewataka watumishi wafanye kazi kulingana na sheria, kanuni na taratibu za kiutumishi na amewakumbusha watumishi kwenda kuchanja chanjo ya ugonjwa wa UVIKO-19.

Akitoa salamu za Wilaya Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Siriel Mchembe amemshukuru Mhe Deogratius Ndejembi kufanya ziara kwenye wilaya ya Handeni na kuongea na watumishi wa Halmashauri zote mbili.

Pia Mkuu wa Wilaya Mhe Siriel Mchembe amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa Kuleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Sindeni kwa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na kituo cha Afya Malezi kilichopo Handeni Mji.

Aidha Mhe. Mchembe amesema madiwani walikuwa wanalipwa kwa fedha za mapato ya ndani lakini kwa sasa serikali kuu imebeba jukumu la kuwalipa madiwani hivyo anaishukuru serikali na kusema kuwa mapato ya ndani kwa kila Halmashauri yatatumika kwenye ujenzi wa miradi ya maendeleo.

Mhe. Deogratius John Ndejembi, Naibu waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora akiongea na watumishi.

Mhe Siriel Mchembe akitoa salamu za Wilaya kwa Naibu waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya  Handeni Bw. Saitoti Zelothe Stephe, akiongea kwenye kikao hiko.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Handeni Mji Bi. Mariamu Ukwaju Masebu akitoa tarifa ya Halmashauri yake.

Mtumishi kutoka kada ya afya akitoa changamoto zake kwa naibu waziri.

Watumishi wakimsikiliza Naibu waziri.

Tangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO KWA WALIOFAULU USAILI KATIKA NAFASI ZA MWENDESHAJI WA KIFAA CHA BAYOMETRIKI NA AFISA MWANDIKISHAJI MSAIDIZI February 20, 2025
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • HANDENI DC IMEFANYA KIKAO CHA BARAZA KWA ROBO YA NNE YA MWAKA 2023/2024

    August 12, 2024
  • WANAWAKE HANDENI WAMPONGEZI DKT. SAMIA

    August 09, 2024
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA

    August 06, 2024
  • KUPITIA MAPATO YA NDANI, HANDENI IMETEKELEZEKA MIRADI KEDEKEDE

    October 23, 2023
  • Angalia zote

Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amalizia ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Kwedikwazu Mashariki.
Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TASAF
  • Fursa za Uwekezaji

Kurasa Mashuhuri

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Tume ya Ajira
  • Ikulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa