Timu hiyo iliyoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe ilifanya ziara ya kukagua mirandi mbalimbali iliyopo kwenye Halmashauri ikiwepo ujenzi wa jengo la makao makuu ya Halmashauri, ujenzi wa vyoo vya shule ya msingi Tuliani, Mradi wa kupanda miti katika kijiji cha Kwamkunga na kiwanda cha kuchakata muhogo pamoja na kusikiliza kero za wanachi
Mkurugenzi Mtendaji Bw. William Makufwe amesema kuwa wao kama wafanyakazi wa Hamashauri wamejiwekea utaratibu wa kutembelea miradi inayoelendelea kutekelezwa kwenye Halamshauri yake ili kuona mwenendo mzima wa maendeleo ya miradi hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe alimpongeza Mkurugenzi mtendaji pamoja na wafanyakazi wa halmashauri ya wilaya ya Handeni kwa kutimiza agizo la Waziri Mkuu la kutoka ofisini kwenda kukagua miradi na kusikiliza kero mbalimbali za wanachi.
Pia Mkuu wa Wilaya Mh. Godwin Gongwe amemuomba Meneja wa wakala wa barabara za mijini na vijijini (TARURA) mkoa wa Tanga Injinia George Tarimo kuirekebisha barabara inayoelekea kwenye jengo la Halmashauri ya Handeni ili magari yanayopeleka vifaa vya ujenzi yaweze kupita.
Na ameagiza kuwa misaragambo yote ya kurekebisha barabara ikifanyika watu wa TARURA lazima wawepo maana wao ndiyo wataalamu wa kutoa ushauri namna ya kurekebisha barabara hizo.
Alihitimisha kwa kuwaagiza wakala wa barabara mijini na vijijini (TARURA) Handeni, Idara ya Ardhi, Mipango miji na idara ya misitu kukaa kikao ndani ya siku kumi ili kuandaa mpango kazi wa makazi ya kisasa.
Kwa upande wa Meneja wa wakala wa barabara mijini na vijijini (TARURA) mkoa wa Tanga injinia George Tarimo amesema atalifanyia kazi suala la kutengeneza barabara ili magari yaweze kupeleka vifaa kwa urahisi katika eneo la ujenzi wa jengo la makao makuu ya Halmashauri.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni Mwl. Boniphace Maiga alishauri kila barabara apewe injia mmoja ili iwe rahisi kufuatilia katika uboreshaji wa barabara hizo.
Mkurugenzi Mtendaji Bw. Wiliiam Makufwe alimueleza Mh. Mkuu wa wilaya pamoja na kamati nzima ya ulinzi na usalama ya wilaya kuwa mpaka sasa ujenzi umefikia 15% pamoja na kuwa na changamoto ya mvua na ubovu wa barabara yenye urefu wa Kilomita 1.5 kutoka barabara kuu kupitisha vifaa mpaka eneo la ujenzi wa makao makuu ya Halmshauri.
Akisikiliza na kutatua kero za wananchi katika kijiji cha Kwamkunga Mkurugenzi Mtendaji kuhusu suala la maji amewaeleza kuwa wataalamu wa maji watakwenda kufanaya tathimini ya mabomba na gharama na kuona namna ya kufikisha maji kijijini hapo, na kwa upande wa umeme amesema tathimini imeshafanyika tayari mradi wa umeme utafika kwamkunga.
Kuhusu kero ya zahanati Makufwe amewaagiza wanakijiji hao kuwa mpaka mwezi wa tisa wawe wamefyatua matofali ya kuchoma elfu kumi na tano (15,000) ili ujenzi wa zahanati uanze mara moja kijijini hapo halafu Halmashsuri inakwenda kumalizia.
Wakati wakikagua shamba la miti la ekari mia moja (100) lililopo kijiji cha Kwamkunga Afisa misitu wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bw. Elinihaki Hashim Mdee alisema wamepata msaada wa fedha kutoka mfuko wa Misitu Tanzania kiasi cha milioni 93 kwaajili ya kuboresha misitu na ekari 50 za shamba zimeshasafishwa tayari kwa kupanda miti.
Kwaniaba ya wananchi wa kijiji cha Kwamkunga, Kata wa Kwankonje Diwani wa kata hiyo Mh.Jonathan Maturu alishukuru timu ya menejimenti ya Halmashauri ya Handeni kwa kufika kijijini hapo na kusikiliza kero za wananchi wa Kwamkunga na kupata majibu ya kuridhisha, pia alisema wananchi wameukubali na kuupokea mradi mkubwa wa miti na kuahidi kutoa ushirikaino.
Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe wa kwanza kulia akipokea taarifa ya ujenzi wa jengo la makao makuu ya Halmashauri kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Bw. Wiliiam Makufwe wa kwanza kushoto.
Mh. Godwin Gondwe mwenyemiwani kulia akimuagiza meneja wa wakala wa barabara mijini na vijijini (TARURA) wa Halamashauri ya Handeni wa pili kushoto kurekebisha barabara inayoanzia sheli ya mogas kuelekea Mhalango ziliko ofisi za Halmashauri.
Katibu tawala Wilaya ya Handeni Mwl. Boniphace Maiga katikati akitoa maelekezo kwa wataalamu wa barabara katika ziara hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halamshauri ya Handeni Bw. William Makufwe aliyenyanyua mkono, akitoa maelekezo katika ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri.
Bw. William Makufwe watatu kulia akiongea na wafanyakazi wa shamba la miti Kwamkunga.
Afisa utumishi Bi. Fatuma Kalovya katikati akifafanua jambo wakati wa ziara hiyo.
Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni wakiwa eneo la ujenzi wamakao makuu ya Halmashauri.
Jengo la makao makuu ya Halamashauri ya Wilaya ya Handeni likiendelea kujengwa.
Shughuli za uchimbaji wa mashimo zikiendelea kwenye shamba la miti Kwamkunga.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa