Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni (CMT) imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye Halmashauri ya Handeni.
Mwenyekiti wa timu ya Menejimenti hiyo Bw. Saitoti Zelothe Stephane ameongoza wajumbe wa timu hiyo amabao ni wakuu wa Idara na vitengo kukagua miradi ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 unaotekeleza ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imepokea kiasi cha bilioni 1.44 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 72 vya madarasa kwa shule za Sekondari na Kiasi cha milioni 380 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 19 za shule za Msingi shikizi. Katika utekelezaji wa Mpango huo Halmashauri ya Wilaya ya Handeni wameupa jina mpango huo kuwa kazi iendelee program.
Katika ziara hiyo timu ya Menejimenti imeridhishwa na ujenzi wa Madarasa hayo na imejipanga kikamilifu kusimamia miradi yote kwa kuzingatia ubora, muda wa utekelezaji na nidhamu katika utekelezaji wa ujenzi wa madarasa hayo na kwa sasa ujenzi wa madarasa hayo yako hatua ya lenta na upauaji.
Mkurugenzi Mtendaji Bw. Saitoti Zelothe Stephen akimwagilia maji kwenye jamvi,Shule ya Sekondari Pangambili alipoogoza CMT kukagua miradi.
Mhandishi John Mshahara wa Halmashauri ya Handeni, kushoto akitoa maelekezo kwa Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari Kwaludege.
Afisa Mipango, Uchumi na Ufuatiliani Bw. Japhet Machumu, kulia akichanganya udongo kwaajili ya ujenzi wa madarasa shule ya Sekondari Kwamgwe.
Muonekano wa ujenzi wa madarasa ya Shule ya Sekondari Segera
Muonekano wa Jengo la madarasa Shule ya Sekondari Pangambili leo tarehe 20/11/2021
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa