Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni umetoa pikipiki mbili zenye thamani ya Shilingi Milioni 4 na laki 5 kwa Watendaji wa Kata za Kwasunga na Kang’ata ikiwa ni maagizo ya Baraza ya kutoa motisha kwa Watendaji hasa wanaofanya vizuri kukusanya mapato na waliopo kwenye mazingira magumu ya kukusanya Mapato .
Motisha hiyo imetolewa leo mara baada ya kumalizika kwa Baraza la Madiwani la kufunga mwaka lililofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Akikabidhi pikipiki hizo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mh. Ramadhani Diliwa amesema kuwa dhamira yao kama Baraza ni kusaidia na kusimamia shughuli za maendeleo na suala zima la ukusanyaji wa mapato katika kata zote.
Ameongeza kuwa Madiwani wanafahamu Halmashauri inakipato kidogo , wangengeweza kugawa pikipiki kwa kata zote 21, lakini ni bora kuanza kuliko kuacha kabisa hivyo lazima Madiwani wote waridhie kama walivyopitisha, maana kwa popote zitakapoenda ni Halmashauri hiihii ya Handeni na sio mwisho mapato yatakapoongezeka pikipiki zitaendeleakununuliwa ili kata zote 21 ziweze kupata.
Aidha amewata Watendajji kuacha kuchukulia kuwa ni mali ya Serikali na kushindwa kutunza, na kwamba Watendaji wanaokabidhiwa wazitunze kama ambavyo wangeweza kutunza za kwao ili ziweze kudumu kwa muda murefu.
“Watendaji nawaeleza pikipiki hizi zisiwe na mikono mingi, muache kufanyia kazi ambazo hazihusiani na malengo yaliyokusudiwa, kama kupakiza mbao, mikaa,magogo na kadhalika msizichoshe mapema, kafanyieni kazi ya Halmashauri ili zidumu kwa muda mrefu na wengine waje waige kutoka kwenu” Amesema Mh. Diliwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bw. William Makufwe amesema kuwa wametimiza maagizo waliyopewa na Baraza ya kutoa motisha kwa watendaji watakaofanya vizuri kwenye kukusanya mapato na walio na waliopo katika mazingira magumu hususani pembezoni ambao wanapata chanamoto kubwa ya kukusanya mapato.
Aidha ameeleza kuwa pikipiki hizo ni mali ya Halmashauri na Kata huika na sio mali ya Mtendaji Kata,lengo ni kusaidia katika shughuli za kukusanya mapato na shughuli nyingine za kiutawala hivyo matumizi Binafsi Hayaruhusiwi.
Ameongeza kuwa motisha zitaendelea kutolewa kadri fedha zitakapopatikana na Kwamba lengo la Halmashauri ni kuhakikisha Watendaji wote wanapata vitendea kazi ambavyo vitasaidia kuongeza ufanisi wa kazi wakati wowote.
Kwaupande wao watendaji wa Kata za Kwasunga na Kang’ata wamepokea kwa furaha vitendea kazi hivyo na kusema kwamba zitawasaidia kufanya kazi kwa weledi na mtawanyiko mkubwa kwenye maeneo yao hali ambayo itapunguza changamoto za ufuatiliaji wa shughuli za mapato na kiutawala katika maeneo yao. Wametoa rai kwa Watendaji wenzao kuongeza juhudi katika kutenda kazi kwa weledi na uadilifu ili kufikia malengo ya Halmashauri.
Mtendaji Kata ya Kwasunga kushoto na Mtendaji Kata ya Kang'ata kulia wakiwa na pikipiki zao mara baada ya kukabidhiwa.
Pikipiki zilizokabidhiwa
Mh.Diwani Kata ya Kabuku ndani aliyeketi kwenye pikipiki kuonyesha wameziokea kwa furaha
Waheshimiwa madiwani wakipokea pikipiki kwa furaha
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wiaya ya Handeni Bw. William Makufwe mwenye joho la Blue akizungumza na Madiwani.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa