Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Martine Shigella amewataka wafanyakazi wa Zahanati ya Komkonga kutumia vifaa vilivyonunuliwa kwa fedha iliyotolewa na Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli tarehe 3/8/2017 alipofanya ziara Mkoani Tanga, kwa kuzingatia maadili ya kazi na kuhakikisha wananchi wanahudumiwa kwa upendo na lugha nzuri bila kuwepo kwa dalili za udokozi na wizi wowote .
Rai hiyo ameitoa jana alipokuwa akikabidhi vifaa vilivyonunuliwa kwaajili ya kuboresha matibabu ya wananchi wa Kata ya Komkonga na kusema kuwa fedha alizoziahidi Rais kiasi cha Milioni 10 zilitolewa mapema Kabla ya kuondoka mara baada ya kumaliza ziara yake.
Aliongeza kuwa kwasababu zilikuwa ni fedha za umma hivyo taratibu za manunuzi zilipaswa kufuatwa ambapo Halmashauri ya Wilaya ilifuata kwa kuagiza vifaa hivyo kwenye bohari kubwa ya dawa na vifaa tiba ya MSD(Medical Stores Department),ambapo baadhi ya vifaa vilipatikana na vingine ilibidi viagizwe kutoka sehemu nyingine kutokana na MSD kutojitosheleza kwa kuwa na vifaa vyote.
Alisema kuwa manunuzi yamekamilika na vifaa vyote vilivyohitajika vimekamilika ndiyo maana vimekabidhiwa na Kumshukuru Rais kwa upendo wake aliouonesha kwa wananchi wa Tanga hususani Handeni Kata ya Komkonga, kwasababu upatikanaji wa vifaa hivyo utawasaidia kuondokana na tatizo lililokuwa sugu katika Zahanati ambako ndipo huduma za matibabu zinatolewa.
Aidha alipongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na wananchi wa Kata ya Komkonga kwa namna ambavyo wamejitoa kwaajili ya kujenga maabara ndogo inayotarajiwa kumalizika baada ya siku nne, itakayokuwa inatumika kuhifadhia vifaa kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia usalama wa uhakika.
Wakati huhohuo amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kupitia taratibu za madaktari kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja anafuatilia na kujiridhisha juu ya tuhuma zinazomkabili Daktari wa Zahanati ya Komkonga, zilizotolewa dhidi yake na wananchi ili kama kuna ukweli hatua zichukuliwe na kupewa onyo, na kama akiendelea afukuzwe kazi sababu Serikali haiwezi kumvumilia mtu ambaye anajifanya ni Mungu mtu.
“Marufuku kwa mtumishi yeyote wa umma kumhudumia mwananchi kwa lugha ambayo haina staha,yeyote atakayebainika kukiuka agizo hili aripotiwe kwa Viongozi wa Wilaya na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ili hatua zitachukuliwa, Kila mtu anahitaji kuheshimiwa na kuthaminiwa utu wake” alisema Mkuu wa Mkoa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe alishukuru kwa mapokezi ya vifaa hivyo na kuahidi kushirikiana na Ungozi wa Halmashauri katika kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa yanafikiwa.
Akisoma taarifa ya vifaa vilivyonunuliwa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Dk.Credeanus Mgimba alisema vifaa hivyo ni pamoja na Vitendanishi vya kupimia taiphodi, mashine ya kuchanganyia sampuli mbalimbali, hadubini, mashine ya kupima wingi wa damu pamoja na vitendanishi vyake ambavyo vimepatikana kupitia fedha za Wizara ya Afya, mashine ya kupimia magonjwa yatokanayo na mkojo na vitendanishi vya kupimia magonjwa ya mkojo, ambapo vimegharimu Tsh.5,296,300/= na kubakiwa na bakaa la Tsh.4,370,000/= iliyopo MSD Tanga itakayokuwa inatumika kuagizia vitendanishi ambavyo vinaukomo kwa kuletwa kwa awamu sababu matumizi yake ni ya taratibu.
Mkurugenzi Mtendaji Bw.William Makufwe aliyevaa shati la draft nyeusi na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe aliyevaa shati la draft nyeupe wakisikiliza wananchi wa Komkonga namna walivyohamasika kushiriki nguvu kazi ya ujenzi wa maabara ndogo ya Zahanati yao.
Jengo la maabara ndogo likiwa linaendelea kwa ujenzi wakati Halmashuri ya Wilaya ya Handeni imechangia kiasi cha Milioni 3.5 kwajili ya umaliziaji na wananchi wa komkonga wakishiriki nguvu kazi na kuleta baadhi ya vifaa kama michanga na kokoto.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya HANDENI Bw. William Makufwe akieleza namna alivyoshirikiana na kamati ya Zahanati na viongozi wa Kata katika kuhakikisha wanapata maabara ndogo ya kuhifadhia vifaa.
Viongozi wakisikiliza kwa makini taarifa ya vifaa vilivyonunuliwa kwaaajili ya kuboresha huduma za matibabu kwenye Zahanati ya Komkonga.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Dk. Credeanus Mgimba akisoma taarifa ya vifaa vilivyonunuliwa.
Mkurugenzi Mtendaji Bw. William Makufwe akisaidiana na mganga mkuu katikati na mKuu wa Mkoa kutoa hadubini tayari kwa kuikabidhi kwa viongozi wa Komkonga.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mh. Ramadhani Diliwa akishukuru kwa kuletewa vifaa vitakavyosaidia kuboresha huduma ya Afya kwa wananchi wa Komkonga na kupunguza adha ya kufata hudduma hizo maeneo ya Mkata na Handeni.
Mkuuwa Mkoa wa Tanga Mh. Martine Shigella akionesha hadubini kwa wananchi kwa lengo la kuboresha afya.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Komkonga Bw.Omary Mngazija akishangilia kupokea hadubini ikiwa ni moja ya kifaa alichokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Martine Shigella mwenye suti ya kijivu kwaajili ya kuboresha huduma za Zahanati ya Komkonga.
Baadhi ya Wananchi wa Komkonga.
Mkuuwa Mkoa wa Tanga Mh.Martine Shigela akizungumza na watumishi na wananchi wa Komkonga juu ya utunzaji wa vifaa hivyo na kupongeza uongozi wa Halmashuri kwa ujenzi wa maabara ndogo.
Mkuu wa Mkao wa Tanga Mh.Martin Shigella akikabidhi hadumini kwa mwenyekiti wa Kijiji cha Komkonga Bw.Omry Mngazija.
Katibu Tawala Mkoa Bi.Zena Saidi akisalimia wananchi wa Kata ya Komkonga.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa