Vikundi vitano vya biashara vyawakilisha Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwenye maonesho ya biashara TAN-TRADE yanayofanyika mkoani Tanga.
Lengo LA maonesho hayo ni kuzitangaza fursa za viwanda, biashara na uwekezaji zinazopatikana mkoani Tanga Katika kuijenga Tanzania ya Viwanda.
Pili ni kujengea uwezo wajasiliamali waliopo mkoani Tanga Katika kutafuta masoko na kuzitangaza bidhaa zao.
Halmashauri zote 11 za mkoa wa Tanga, taasisi za serikali, Viwanda vyote vilivyopo Tanga vimeshiriki
Maonesho hayo Yameanza Tarehe 28/5 hadi 6/6 2017 na vikundi vilivyowakilisha Halmashauri ya Wilaya ya Handeni ni pamoja na Mkaliatabu cha Kata ya Kitumbi, Jumukulu cha Kata ya Mkata, Jiongeze cha Kata ya Mazingara, balalu cha Kata ya Misima na Uwamta cha Kata ya Mkata.
Wananchi wote mnakaribishwa kutembelea banda LA Halmashauri ya Wilaya ya Handeni. Maonesho hayo yanafanyika Mwahako grounds.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa